Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema huduma ya umeme imerejea saa 7.11 mchana nchi nzima isipokuwa mkoa wa Mbeya.
Huduma ya umeme ilikatika tangu jana katika mikoa yote iliyounganishwa katika gridi ya taifa.
Taarifa
iliyotolewa leo Ijumaa mchana, Desemba 1, 2017 na Kaimu Meneja
Mawasiliano wa Tanesco, Leila Mhaji imesema mkoa wa Mbeya ndiyo pekee
ambao huduma hiyo haijarejea kutokana na hitilafu iliyopo katika njia ya
Mufindi.
Amesema
mafundi wanaendelea kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kwamba
huduma hiyo inarejea katika mkoa huo kama ilivyo kwenye mikoa mingine.
“Tutaendelea kuwajulisha mara huduma hiyo itakaporudi kwani mafundi wanaendelea na kazi,” amesema.
Amesema mapema leo huduma hiyo ilianza kurejea katika mikoa ya Iringa, Dodoma na Tanga
Amewaomba
radhi wateja kwa usumbufu wowote uliojitokeza. Amesisitiza wananchi
kutoshika wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.
0 comments: