JOSEPH YONA HAIKUBALIKI KUWAKUMBATIA WABADHIRIFU


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi tawi la bokorani Mh Joseph Yona amesema naunga mkono jitihada za Rais na Mwenyekiti wa ccm Taifa Mh John Magufuli katika kulinda na kusimamia mali za Nchi na chama

Alisema ilifika sehemu nchi hii ikawa pango la walanguzi kila mtu anafanya kivyake sasa basi ubadhilifu ndani ya nchi hii marufuku tunataka Taifa lenye kuendeshwa katika misingi na sheria tulizo jiwekea 

Joseph Yona alisema kila mtu awajibike katika nafasi yake mimi nitawajibika katika tawi langu na kila mmoja awajibike katika nafasi yake 

Mh Yona alisema kuwa sita mfumbia macho yeyeto atakae shindwa kuzilinda mali za chama katika mazingira yangu hata awena nafasi kiasi gani

Mh Joseph Yona aliyasema hayo leo katika kikao cha mkutano mkuu wa kata ya mtoni kilichofanyika katika ukumbi wa ccm mtoni

Mh Yona Akichangia mada mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa kata ya mtoni 

Wajumbe wa mkutano mkuu wa kata ya mtoni wakisikiliza hoja ya Mh joseph Yona

Mh MPUTA AMESEMA MAGUFULI KATUFANYA TUTEMBEE KIFUA MBELE

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm kata ya mtoni Mh Mputa Zeno Maokola  amejikuta kushindwa kujizuia hisia zake juu ya Rais na Mwenyekiti wa ccm Taifa Dr Magufuli

 Mh MPUTA amesema saivi Magufuli kutufanya tutembee kufua wazi na jezi zetu za chama mtaani bila woga kwani yanayotendeka na Mwenyekiti wa Chama ni makubwa na niyakujivunia aidha Mwenyekiti huyo alisema kwa juhudi zake yeye na uongozi wake hayo kubali kuipoteza kata tena mikononi mwa wapinzani na kuahidi kushughulikia aina yoyote ya makundi ndani ya chama sisi sote kundi letu ni ccm

Mh Mputa amepinga vikali matumizi mabovu ya madaraka kwa viongozi wa chama kuanzia Ngazi yake mpaka katika Mashina tuwahudumie wananchi maana ndio waajiri wetu tufanye kazi katika mazingira ya kuheshimu haki na misingi ya utawala bora

Mh Mputa aliyasema hayo leo katika kikao nawajumbe wa mkutano mkuu kata ikiwa ni mkimbisho wa watendaji wote dani ya kata kutoka katika matawi yote na mashina ndani ya Mtoni
Pichani ni wajumbe wa mkutano mkuu wa kata wakisikiliza yale yaliyo pagwa kufanywa na uongozi waMh Mputa
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi tawi la bokorani Joseph Yona alichangia msaada katika kikao

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya January 3


Spika Ndugai Amjibu Tundu Lissu


Spika  wa Bunge Job Ndugai amefunguka na kusema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu pamoja na familia yake hawatambui kuwa Serikali hasa Bunge limeanza kufanya mazungumzo na watu wanaotaka kumsafirisha kwenda nje kwa matibabu zaidi.

Ndugai amedai anatambua kuwa Tundu Lissu atasafirishwa na kwenda kwa matibabu zaidi nje ya Kenya ingawa hajajua ni lini lakini amesema kuwa watu ambao wamepanga kumpeleka huko kwenye matibabu tayari walishamtafuta yeye na kusema watashirikiana nao katika masuala ya matibabu.

"Ni kweli kwamba atapelekwa nje zaidi ya Nairobi ila bado sijui mpaka sasa ni lini kwa kuwa sijajua tarehe bado japo nadhani itakuwa hivi karibuni na wale wanaomgharamia kumpeleka nje wameshawasiliana na mimi na hakika familia ya Lissu hata Tundu Lissu mwenyewe hajui hilo, anafikiri ni wao peke yao lakini najua na walishafika kwangu na kusema watagharamia wao" alisema Ndugai

Spika Ndugai alizidi kueleza kuwa endapo watakubaliana na watu hao basi wao kama Serikali watagharamia katika mambo mengine ambayo yatawashinda hao wadau ambao walimfuata na kuongea naye.

"Gharama ambazo sisi tunaweza kuziingia endapo tutakubaliana na maamuzi hayo kufanyika itakuwa katika yale mambo mengine yanayobakia ambao wale kama wadau, wawezeshaji, wanaotusaidia hawataweza kutoa na ili liafikiwe lazima tuwe na uhakika kitu gani kinalipiwa na kitu gani hakilipiwi vinginevyo tutalipa mara mbili mbili sisi tunalipa wenzetu wanalipa ambapo kidogo italeta mchanganyiko usiokua na afya" alisisitiza Ndugai

Mwaka jana Tundu Lissu alidai kuwa Serikali pamoja na Bunge bado walikuwa hajachangia jambo lolote katika matibabu yake ambayo yanaendelea mpaka sasa nchini Kenya jijini Nairobi kufuatia shambulio lake la kupigwa risasi Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.

Umoja wa mataifa washusha Rungu kwa rais wa congo (DRC)




Umoja wa Mataifa umemwambia Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila kutimiza ahadi aliyoiweka ya kuachia madaraka na kupisha uongozi mwingine kuiongoza nchi hiyo hususani wakati huu ambapo nchi hiyo imejaa migomo na maandamano ya kushinikiza ajiuzulu.

Rais Kabila mwenye miaka 46, ameiongoza DRC kwa miaka 17 na msimu wake wa mwisho wa uongozi uliisha tangu December 31, 2016 na akatakiwa aachie ngazi lakini uchaguzi wa kupata Rais na viongoi wapya umekuwa ukiahirishwa mara kwa mara.

Suala hili limesababisha vurugu na maandamano ya raia wa DRC ambao hata hivyo inaelezwa kuwa wamekuwa wakipigwa na askari polisi jamabo ambalo kwenye taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa December 31, 2017 imelaani vikali vitendo hivyo hususani Jijini Kinshasa ambapo watu watano waliuawa na polisi siku hiyo vya Jumapili kwenye maandamano.

TRA Wakomaa na Askofu Kakobe.....Wadai Hawana muda wa Kubishana nae Zaidi ya Kuchunguza Utajiri wake



Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imemuibukia kivingine, Askofu wa Kanisa la Full Gosper Bible Fellowship (FGBF), Zakaria Kakobe, kuhusu utajiri alionao ikisema haina muda wa kulumbana naye, bali inatekeleza maelekezo ya Kamishna Mkuu.

Aidha, mamlaka hiyo imesema haitaki kuwa kwenye malumbano na askofu huyo wakati ikiendelea na uchunguzi dhidi ya vitega uchumi vyake na kuangalia kama analipa kodi ya serikali.

Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo, jana alisema maofisa wao wanaendelea kutekeleza tamko la Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere, la kuchunguza utajiri wa Askofu Kakobe.

"Sisi (TRA) hatutaki kuwa kwenye malumbano na Kakoke, tulichosema tumeishia hapo. Alichosema Kamishna Mkuu tunaishia hapohapo, hatutakiwi kujibishana naye," Kayombo alisema.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumamosi, Kichere alisema mamlaka yake imeipokea kwa furaha kauli ya Askofu Kakobe kuhusu utajiri wake na inataka kujiridhisha vyanzo vya utajiri huo.

Kichere alisema TRA inafahamu kuwa shughuli za kidini hazitozwi kodi, lakini inataka kufahamu kama fedha hizo za Askofu Kakobe zinatokana na sadaka pekee.

Alisema wameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na kiongozi huyo wa kiroho kutokuwamo katika kumbukumbu za ulipaji kodi za TRA.

Kauli iliyoleta utata na kuibua uchunguzi huo ni ya Askofu Kakobe kukaririwa wiki iliyopita akidai ana fedha nyingi kuliko serikali na anao uwezo wa kumkopesha waziri pindi akiombwa kufanya hivyo.

Hata hivyo, juzi ikiwa ni siku moja baada ya TRA kutangaza kufanya uchunguzi dhidi yake, Askofu Kakobe alieleza historia ya maisha yake, mali za kanisa na zake na misukosuko aliyopitia na kusisitiza kuwa tafsiri iliyofanyika dhidi ya kauli yake kuhusu utajiri ni ya kimwili na siyo ya kiroho. Alidai kauli yake ilimaanisha yeye ni tajiri wa kiroho na si fedha.

Askofu Kakobe aliishauri TRA kutohangaika naye, badala yake ikatafute fedha mahali kwingine akieleza kuwa ana nyumba moja iliyopo Kijitonyama jijini na aliijenga mwaka 1986 kwa gharama ya Sh. milioni mbili ikiwa ni pamoja na gharama za kiwanja.

Huku akishangiliwa na waumini wa kanisa lake kwenye ibada ya kuuaga mwaka 2017, Askofu Kakobe pia alidai kuwa mwaka 1995 alinunua gari aina ya Nissan Patrol kwa kutumia sadaka za washirika wa kanisa na hivi karibuni waliibuka watu waliochangishana na kumnunulia gari jingine.

Alidai kuwa hata kwao Kakonko, Kigoma hajawahi kujenga hata choo na kilichopo ni makaburi ya wazazi wake waliozikwa kwenye eneo la kuingia kwenye nyumba iliyojengwa na wazazi wao.

Askofu Kakobe pia alidai kuwa kanisa la FGBF ndani na nje ya nchi halina mradi wowote wa kiuchumi kama shamba au hoteli na akasisitiza serikali ichunguze kote huko.

Alibainisha kuwa makusanyo yote ya sadaka huhifadhiwa kwenye akaunti iliyofunguliwa mwaka 1990 katika Benki ya NBC na ni mali ya bodi ya wadhamini ambayo imesajiliwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita).

Breaking News: Televisheni 5 Nchini Zapigwa Faini na TCRA kwa Kukiuka Maadili ya Utangazaji


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA, imevipiga faini vituo vitano vya Televisheni  kwa makosa ya ukiukwaji wa taratibu za kutangaza taarifa ya habari hapa nchini.

Adhabu hiyo imetangazwa leo na Makamu mwenyekiti wa kamati  ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) , Joseph Mapunda

Kituo cha runinga cha EATV, kimetozwa faini ya jumla ya TZS milioni 15, kwa makosa matatu ikiwemo, kukiuka maadili ya uandishi na kutangaza habari za uchochezi. Faini hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30, na kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi 6.

Aidha, TCRA imekitoza faini ya TZS milioni 15 kituo cha Runinga cha Channel ten, kwa makosa ya kutangaza habari ambazo hazikuzingatia maadili ya uandishi, kutangaza habari za uchochezi, na kutozingatia mizania. Pia kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa miezi sita kuanzia leo.

Kituo cha runinga cha Star TV, kimetozwa faini ya jumla ya TZS milioni 7.5 kwa makosa matatu ikiwemo, kukiuka maadili ya uandishi na kutangaza habari za uchochezi. Faini hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30 na pia kituo hicho kinawekwa chini ya uangalizi wa miezi 6.

Pia TCRA imekitoza faini ya TZS milioni 7.5 kituo cha runinga cha Azam Two, kwa makosa ya kutangaza habari za uchochezi, kutangaza habari ambazo hazikuzingatia maadili ya uandishi na kutozingatia mizania. Pia kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa miezi sita kuanzia leo. 

Kituo cha runinga cha ITV, kimetozwa faini ya jumla ya TZS milioni 15, kwa makosa matatu ikiwemo, kukiuka maadili ya uandishi na kutangaza habari za uchochezi. Faini hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30, na kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi 6.