Moto Israel: Washukiwa 12 wakamatwa

Maafisa wa polisi nchini Israel wamewakamata watu 12 kwa tuhuma za uchomaji wa makusudi kufuatia msururu wa moto ambao umekuwa ukilichoma taifa hilo kwa siku nne sasa.
Zima moto wameudhibiti moto huo katika mji wa kaskazini wa Haifa ambapo takriban watu 80,000 walilazimishwa kuondoka.Waziri mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuWaziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Lakini maafisa wanasema moto midogo midogo bado inaendelea kukabiliwa katika maeneo tofauti.
Netanyahu: Moto mkubwa Israel umesababishwa makusudi
Moto huo umesababishwa na hali ya kiangazi pamoja na upepo mkali.
Watu kadhaa wametibiwa kwa kuvuta moshi lakini hakuna majeraha yalioripotiwa.


Waziri mkuu wa Israel awali alisema kuwa iwapo moto huo ulianzishwa kwa makusudi basi washukiwa watakabiliwa na mashtaka ya ugaidi
Kwa Picha: Moto mkubwa watishia Israel
Waziri wa elimu Naftali Bennet ,kiongozi wa chama cha Jewish Home Party ,aliashiria kwamba huenda kuna mkono wa Waarabu ama Wapalestina kupitia ujumbe wake wa Twitter uliosoma: Ni wale wasiotoka katika taifa hili ambao wanaweza kulichoma pekee.
Vuguvugu la rais wa Palestina Mahmoud Abbas, Fatah limesema kuwa maafisa wa Israel wanatumia moto huo kuwalaumu Wapalestina.

Share on Google Plus

0 comments: