Shirika la Ndege la Etihad laingia makubaliano ya Kihistoria na 'Precision Air'
KATIKA
hatua za kuhakikisha inayafikia maeneo mengi Afrika Mashariki, Shirika
la Etihad la Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu limeingia makubaliano na
Shirika la ndege la hapa nchini Precision Air ambayo yamelenga kupanua
huduma zaidi ndani na nje ya Tanzania.
Makubaliano
hayo yanatoa fursa kwa, Shirika la Ndege la ‘Precision Air’ ambalo
linaongoza kwa utoaji huduma hapa nchini kuweza kutoa huduma za moja kwa
moja katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu na zaidi.
Kupitia
makubaliano hayo, Shirika la Ndege la Etihad litaweka alama yake ya
kibali EY kwenye ndege za ‘Precision Air’ zinatoa huduma kati ya Dar es
Salaam, Kilimanjaro, Mwanza, Mtwara, Nairobi, Zanzibar na Pemba,
Vilevile kwenye ndege zinazotoa huduma kati ya Nairobi, Kilimanjaro na
Zanzibar.
Aidha,
Precision Air pia itaweka alama yake ya PW kwenye Ndege za Etihad
zinazotoa huduma zake za kila siku kati ya Dar es Salaam na Abu Dhabi
ikiwa ni hatua ya kuhimarisha uhusiano kati ya Afrika Mashariki na Falme
za Kiarabu.
Kwa
mujibu wa Ofisa Mkuu wa Mipango na Mikakati wa Shirika la ndege la
Etihad, Kevin Knight, ‘Precision Air’ ni shirika lenye ubunifu wa hali
ya juu ambalo limeweza kuibuka na tuzo mbalimbali katika utoaji wa
huduma bora za anga.
Makubaliano
yetu leo yanadhihirisha kuwa ndoto ya Shirika la Ndege la Etihad ya
kuhimarisha huduma katika Ukanda wa Afrika Mashariki inazidi kukua.
“Huu ni
mfano mzuri zaidi katika kuifikia mipango mikakati yetu ya kufanya kazi
na wadau ili kutimiza dhamira yetu na kutoa huduma bora za kibiashara na
usafiri wenye raha kwa chaguo bora zaidi,” aliongeza Ofisa huyo.
Naye
Sauda Rajabu ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu wa Precision
Air Services PLC, alisema, “Hii ni hatua muhimu na mpya kwa Precision
Air, na tunafurahi sana kufanya kazi na Shirika la Ndege la Etihad
katika ushiriiano huu. Tunatazamia kuwakaribisha abiria wengi zaidi wa
Shirika la ndege la Etihad kwenye ndege zetu na ni furaha yetu kuendelea
kuzifikia fursa nyingi zaidi katika hatua ambayo itasaidia kuhimarisha
uhusiano wetu kwa mipango ya muda mrefu.
“Kwa
kupitia ushirikiano huu, tunawasaidia wateja wetu wa safari za ndani
kujipatia fursa zaidi ya kwenda Abudhabi, na kusafiri maeneo zaidi ya
100 duniani kupitia mtandao mpana wa Shirika la ndege la Etihad ambao ni
Afrika Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Marekani,”
Tangu
jana abiria wameanza kukata tiketi za safari kutoka kwa mawakala au
katika ofisi za mashirika haya kwa ajili ya safari za Januari 11,
mwakani na kuendelea.
Shirika
la Ndege la Etihad kwa sasa linatoa huduma katika nchi kumi barani
Afrika 10 Afrika ikiwemo Johannesburg, Nairobi, Entebbe, Dar es Salaam,
Khartoum, Casablanca, Rabat, Lagos, Cairo na Mahé, Seychelles
0 comments: