Na.Alex Mathias,Dar es salaam
Baada ya
kuona makapuni ya Maegesho ya magari yanaendelea kukeuka masharti na
taratibu za nchi hatimaye Leo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la
Dar es Salaam, Isaya Mwita,ameamua kutolea ufafanuzi pamoja na kutoa
tahadhari kwa makampuni ambayo yamepewa mikataba hiyo.
Akizungumza
na Waandishi wa habari amesema kuwa ameamua kutoa ufafanuzi juu ya
wafanya biashara hao ambao wamekuwa wakikeuka taratibu na kuanza kutoa
tozo kubwa ya ushuru kwa watu ambao wamekuwa wakiegesha magari na
kupandishiwa kodi kwa dakika chache pamoja na kukamata magari hayo na
kuyafunga kamba/
“Ni kweli
nimesikia habari hizo na ndo maana nameona niongee nanyi wanahabari
hivyo naonya mawakala hao wanaofanya kazi kinyume na utaratibu huo na
sasa naangiza kuwa mtu atakaye park gari anatakiwa gari likae dakika 60
bila kusumbuliwa na kama wataendelea kukeuka tutawafutiya lesseni ya
kufanya kazi”amesema Mwita
Hata
hivyo amesema kuwa ifikapo Januari,2017 kwa Makampuni yote kuanza
kutumia tiketi za kielektroniki na kama kuna mawakala au kampuni
watashindwa kutumia hizo tiketi watavunjiwa mikataba na pia anawataka
watu lazima wadai tiketi hizo.
Meya huyu
kuanzia sasa anawataka mawakala kuanza kuwatoza watu ushuru kuwaacha
wateja wao wapark dakika 60 ndipo wapewe Listi ya kuegesha magari huku
wakitumia tiketi za Kielektroniki na mtu asipopewa listi hizo au
kupandishiwa kodi wanatakiwa watoe taarifa kwa jiji la Dar es salaam.
Anamalizia
kwa kusema kuwa anawatakia Krismas njema na kutoa onyo kwa watu ambao
watafanya vurugu watachukuliwa hatua kali na utakuwepo ulinzi wa kutosha
0 comments: