Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu
Hassan amewahimiza wanafunzi kote nchini kupenda kusoma masomo ya
Sayansi hasa watoto wa kike ili Taifa liweze kujitosheleza kwa wataalamu
wa fani mbalimbali nchini hasa wakati huu ambao Taifa linaelekea kwenye
uchumi wa Viwanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika
hotuba yake kwenye mahafali ya Pili ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa
shule ya sekondari ya WAMA- NAKANYAMA Jijini Dar es Salaam, mahafali
ambayo imehudhuriwa na wake wa Marais Wastaafu.
Makamu
wa Rais amesema haitapendeza hata kidogo ajira nyingi nchini
kuchukuliwa na wataalamu mbalimbali mataifa ya nje hasa kipindi hiki
wakati Serikali inahimiza ujenzi wa viwanda hivyo amesisitiza wanafunzi
wajikite kwenye kusoma masomo ya sayansi ili taifa liweze kujitosheleza
kwa ajili ya manufaa ya maendeleo ya taifa. Amesema katika kuhakikisha
taifa lipata wanasayansi wengi, Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi
wa maabara na kununua vifaa vya maabara ili kuhamasisha wanafunzi wengi
zaidi kupenda kusoma masomo ya sayansi kote nchini.
Makamu
wa Rais pia amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano inakusudia
kuimarisha ufundishaji wa masomo ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano
–TEHAMA- katika shule za Sekondari na kujenga maabara za kompyuta nia
ikiwa ni kuongeza wataalamu wa fani hiyo nchini. Kuhusu mila na desturi
kandamizi kwa wanawake na wasichana zilizopo kwenye baadhi ya jamii
nchini, Makamu wa Rais ameitaka jamii kukomesha mila hizo na
iwashirikishe wanawake katika mipango na mikakati ya maendeleo ya nchi
kwani watakuwa ni chachu ya maendeleo katika jamii husika.
“Wote
tunajua wanawake ni chachu na kiungo muhimu katika maendeleo ya jamii,
Taifa na Dunia kwa ujumla hivyo ni wajibu wa jamii kushirikisha wanawake
katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo kote nchini”
amesisitiza Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais pia
ameipongeza Taasisi ya Wanawake na Maendeleo – WAMA- kwa kujenga shule
Mbili za Sekondari na kusomesha watoto wanaotoka kwenye familia maskini
na yatima na kusema huo ni mfano wa kuingwa na wadau wengine wa
maendeleo katika kusaidia kundi hilo ili watoto wanaotoka kwenye familia
maskini nao waweze kuapata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya
baadae.
Kuhusu changamoto
zinazoikabili shule ya WAMA – NAKAYAMA, Makamu wa Rais ameahidi
kushughulikia changamoto hizo ikiwemo uhaba wa maji, ubovu wa barabara
kuelekea kwenye shule hiyo na tatizo la uhaba wa mabweni.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne
Mama SALMA KIKWETE amesema aliamua kuanzisha taasisi hiyo ambayo
inamiliki shule Mbili mpaka sasa ili kusaidia watoto wa maskini na
yatima kupata elimu bure ambapo mpaka sasa kuna idadi kubwa ya wanafunzi
wanaliohitimu katika shule hizo ambao wamejiunga na masomo ya elimu ya
juu.
Mama Salma Kikwete
ameshukuru ushirikiano mkubwa anaopata kutoka Serikalini unaolenga
kuhakikisha shule zinazoendeshwa na taaisisi hiyo ikiwemo ya Wama –
Nakayama zinafanya vizuri.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wengine
wakiangalia kwa vitendo majaribio ya kiyasansi kutoka kwa wanafunzi wa
kidato cha sita wa shule ya sekondari ya WAMA NAKAYAMA kwenye sherehe za
mahafali yao ambapo wanafunzi 45 wamehitimu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete(kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa
WAMA Bi.Zakhia Meghji wakiimba wimbo maalumu wa shule ya Sekondari ya
WAMA NAKAYAMA wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha sita ambapo
wanafunzi 45 wamehitimu.
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondari WAMA NAKAYAMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: