Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Dkt. Susan Kolimba amekutana na kufanya mazunguzo na Mabalozi
Wateule wanaoenda kuiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali
Duniani.Mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Nchi
mjini Dodoma, yalijikita katika kujadili namna bora ya kuiwakilisha
Tanzania ughaibuni kwa kuzingatia sera ya nchi ya mambo ya nje, kwa
lengo la kuboresha mahusiano ya Kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi
hizo, na kwa kuzingatia maslahi mapana ya kiuchumi ya nchi yetu ikiwemo
kutangaza shughuli za utalii zinazopatikana nchini. 
Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan Kolimba akisisitiza jambo

Balozi Mteule Baraka H. Luvanda akichangia jambo wakati wa mazungumzo. Punde baada ya mazungumzo na Mhe. Naibu Waziri, Mabalozi walikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Katibu Mkuu Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Aziz P Mlima akiongea na Mabalozi ofisini kwake mjini Dodoma

Mazunguzo yakiendelea
0 comments: