Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo
amesaini kandarasi zenye thamani ya dola za Marekani Milioni 268.35
ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 600 za Tanzania mjini Tabora kwa
mkopo wa benki ya Exim ya nchini India kwa kushirikiana na Serikali ya
Tanzani kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoa Ziwa Victoria na
kupeleka katika Manispaa ya Tabora na Halmashauri za Igunga, Uyui,
Shinyanga Vijijini na Nzega.
Utekelezaji
wa mradi ni wa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ya Mradi ilikuwa
kufanya usanifu na kuandaa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi,
kazi ambayo ilifanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India na ilikamilika
mwezi Desemba 2015.
Awamu
ya pili ni ujenzi wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu
ya kwanza itaanzia Kijiji cha Solwa (kilichopo Wilaya ya Shinyanga
Vijijini) hadi Mji wa Nzega, ujenzi utafanywa na Kampuni ya Megha
Engineering Infrastructures Ltd ya India. Sehemu ya Pili inaanzia Mjini
Nzega mjini hadi Manispaa ya Tabora kupitia Halmashauri ya Wilaya ya
Uyui, ujenzi utafanywa na Kampuni ya L&T ikishirikiana na kampuni ya
Shriram zote kutoka India.
Sehemu ya tatu
inaanzia Nzega mjini hadi Igunga mjini, ujenzi utafanywa na Kampuni ya
Afcons ikishirikiana na kampuni ya SMC zote kutoka India. Usimamizi wa
mradi unafanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India.
Katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo naVisay Uplenchwar wa Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd akisaini Mikataba ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka kijiji cha Solwa Shinyanga na kupeleka maji Nzega.Mbunge wa Nzega Hussein Bashe akimsalimia waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng. Lwenge
Waziri
wa maji na Umwagiliaji Eng. Gerson Lwenge akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa
Tabora wakati alipowasiri katika viwanja vya Furahisha Tabora.
Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini
About author: PAVEA BLOG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: