Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh.Amos Makalla amepokea msaada wa mifuko 400 ya saruji,kutoka kwa Benki ya AKIBA
Commercial Bank Ltd ,kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa njia za
Wagonjwa,yenye urefu wa mita 175 katika hospitali ya Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza
hayo jana jijini Mbeya wakati wa kupokea msaada huo,RC Makalla
aliwashukuru Wadau hao kwa kujitolea na kulishughulikia ombi lake kwa
haraka na kwa uzito wa juu kabisa.
"Nawashukuru sana Wadau AKIBA
Commercial Bank Ltd , kwa kulishughulikia ombi langu hili, ambalo
sikutarajia kama lingechukua muda mfupi hivi,nawashukuru sana na
nawaomba msichoke na tuendelee kuijenga Mbeya yetu kwa pamoja",alisema
Makalla.
Makala alisema kuwa kupitia
kwa marafiki wa hospitali ya Mkoa,wanaoishi ndani na nje ya mkoa
huo,kupitia harambee walioifanya hivi karibuni wamefanikiwa kukamilisha
ujenzi wa mita 55 na na kuwa awamu ya pili inaendelea kwa ujenzi wa mita
175.
Mh.Makalla alisema kuwa katika
awamu ya kwanza ya ujenzi huo,zilitumika fedha jumla ya shilingi milioni
600,kutokana na mahitaji kuwa makubwa ya ujenzi,ujenzi ukasimama. kwa
sababu zilikuwa zikihitajika fedha nyingine kiasi cha shilingi milioni
55,ndipo wakachukua hatua za kuomba msaada zaidi kwa wadau ambao ni AKIBA Commercial Bank Ltd .
"Kukamilika
kwa ujenzi huu kutaondoa tatizo la wagonjwa kupelekwa au kwenda wodini
kwa taabu, kwani wakati wa mvua tatizo linakuwa kubwa ",alisema Mh
Makalla.
Kwa upande wa Akiba
Commercial Bank kupitia kwa Afisa Masoko na Uendeshaji Bi Dora Saria
amesema waliguswa sana baada ya kuombwa na Mkuu wa Mkoa kutokana na
wananchi kupata shida hasa wagonjwa kwenda wodini au kupeleka maiti
kwenye chumba cha kuhifadhia maiti
Hivyo
wao kama taasisi ya Benki waliguswa na jambo hilo,na wakachukua hatua
ya kuchangia shilingi milioni 5 sawa na Mifuko 400 ya saruji na kuahidi
kutoa Mafunzo na mikopo kwa wajasiriamali
Aidha
Akiba wamevutiwa na jitihada za Mkuu wa Mkoa kuliweka jiji safi hivyo
watatoa Vifaa vya usafi na kushiriki kufanya usafi mwisho wa mwezi huu.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya,Mh.Amos Makalla akikabidhiwa mifuko 400 ya saruji na
Bi. Dora Saria ambaye ni Afisa Masoko wa Akiba Commercial Bank Jijini
Mbeya.Na Mr.Pengo wa Globu ya jamii Mbeya
RC Makalla akitoa neno la shukrani mbele ya Viongozi na wafanyakazi wa Benki ya Akiba na Serikali kwa ujumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: