HATIMAYE HAMISA MOBETTO AWEKA MAMBO HADHARANI
Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameamua kuweka mambo hadharani kwa kumtaja
baba wa mtoto wake wa pili AbdulLatif kuwa ni Diamond Platnumz.
Kwa mujibu wa akaunti ya mtandao wa Instagram ya mtoto huyo inaonyesha
jina kamili la mtoto kuwa ni “Dully Dangote (AbdulLatif Naseeb Abdul
Juma )Lion 🦁 (Leo) -8|8|2017 TanzanianBaby 👑 @hamisamobetto &
Diamond Platnumz Son.”
Miezi kadhaa nyuma Diamond Platnumz alikuwa akikana kuhusika kutoka
kimapenzi na mwanamitindo huyo na pia kukana mimba aliyokuwa nayo mrembo
huyo.
Hamisa ambaye alianza kutaja majina ya baba wa mtoto huyo miezi kadhaa
nyuma kwa herufi za mwanzo, hatimaye ameweka jina lote la baba huyo
katika akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram.
Abdullatif ni mtoto wa pili wa mrembo huyo ambapo mtoto wa kwanza Fantasy alizaa na Mkurugenzi wa EFM, Majay.
0 comments: