JESHI LA POLISI LAKAMATA WASIOJULIKANA WATANO DAR
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limetangaza kuwakamata
watu watano ambao wamekiri kufanya uhalifu na kuvunja katika ofisi ya
Mawakili ya Prime Atorneys iliyopo katika jengo la Prime house, Mtaa wa
Tambaza, Upanga jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa
amefunguka na kusema kuwa jeshi la polisi limeweza kuwakamata watu hao
ambao mwanzo baadhi ya wananchi walikuwa wakisema watu wasiojulikana
ambao walifanya uhalifu huo na kudai wamekiri kuhusika na uvunjaji wa
ofisi hiyo na kuiba.
"Kutokana na msako mkali jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata
watuhumiwa watano kuhusiana na kesi ya uvunjaji wa ofisi ya Mawakili ya
Prime Atorneys mnamo Septemba 12, 2017 jeshi la polisi lilipokea taarifa
ya kuvunjwa kwa ofisi ya mawakili hao ambapo wahalifu hao walifanikiwa
kuvunja na kuiba kasiki iliyokuwa na pesa milioni tatu laki saba,
waliiba kompyuta mpakato mbili pamoja na nyaraka mbalimbali za ofisi
hiyo na wateja" alisema Lazaro Mambosasa
Aidha Kamanda Mambosasa aliendelea kusema kuwa kutokana na msako mkali
uliofanywa na jeshi la polisi uliweza kuwakamata watu watano ambao
waliwataja kuwa ni pamoja na "Said Idrisa Salehe (47), Mustapha Ibrahim
Said (35), Somvi M Somvi (52), Imani Bago Mhina (36) na mshtakiwa na
watano ni Husein Hajib Suleman (45) baada ya mahojiano na watuhumiwa hao
wote wamekiri kuhusika na tukio hilo na kuonyesha Kasiki la fedha
pamoja na mitungi mitatu ya gas iliyotumika kuvunja ofisi hiyo" alisema
Mambosasa
Aidha Mambosasa amewataka Watanzania pamoja na viongozi mbalimbali kuwa
wavumilivu pundu tukio linapotokea na kutoa nafasi kwa jeshi la polisi
kuweza kufanya uchunguzi na upelelezi wake wa kina kuwapata wahalifu
wanaokuwa wamehusika kwenye matukio hayo.
"Kwa hiyo masihara mengine yanayofanywa na Watanzania yanalenga
kupotosha ukweli lakini pia wanajaribu kuingilia upelelezi wa polisi ili
ukweli usijulikane sote sasa tunashuhuda tulianza kwa kutowafahamu
mashuhuda lakini upelelezi wa kina umefanyika na tumewapata kwa majina
na wao wenyewe wamekiri kufanya matukio hayo, sasa nimualike aliyekuwa
akipotisha Watanzania kwa nguvu kuwa aliyetenda kosa hilo hajulikani aje
sasa atueleze kuwa na yeye ni miongoni mwa waliotenda makosa hayo kwa
sababu tayari hawa wapo na wamekiri kufanya makosa hayo" alisisitiza
Mambosasa
0 comments: