JAJI MKUU ALIYEFUTA UCHAGUZI KENYA AFUNGUKA KUHUSU VITISHO
Jaji
Mkuu wa Kenya, David Maranga amesema tangu kutolewa kwa uamuzi wa
kubatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, mhimili huo umekuwa
ukitishiwa.
Kupitia tamko lake kwa umma, Jaji Maranga ameeleza kuwa kumekuwa na
vitendo vya kuitishia mahakama kwa kufanya maandamano yanayoambatana na
vitendo viovu.
“Maandamano yamejikita katika vitendo viovu na vurugu, vinaonesha wazi kuwa vinalenga kuitishia Mahakama,” alieleza.
Tamko hilo limekuja kufuatia maandamano makubwa yanayofanyika katika
maeneo mbalimbali nchini humo kupinga uamuzi huo wa Mahakama
uliobatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta uliokuwa umetangazwa na
Tume Huru ya Uchaguzi ya IEBC.
Katika uamuzi wake, Mahakama ilieleza kuwa uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi na kwamba haukuwa wa haki.
Kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama uliozingatia Katiba ya nchi hiyo,
uchaguzi wa marudio unapaswa kufanywa Oktoba 17 mwaka huu ukisimamiwa na
IEBC.
Hata hivyo, upande wa NASA ukiongozwa na Raila Odinga, ambao umeshinda
kesi hiyo umeendelea kupinga IEBC kuandaa tena uchaguzi huo wakidai ni
wahalifu ambao wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na sio kupewa
kazi nyingine.
0 comments: