TUSIPOKUWA MAKINI MAADUI ZETU WATAFANIKIWA KUHARIBU UMOJA WETU.
NA
Joseph yona
Kwanza kabisa nianze kwa kusema nimeumizwa sana na shambulio la silaha alilofanyiwa Ndugu yetu, Mh. TUNDU ANTIPAS LISU, na kumsababishia majeraha makubwa sana. Jambo hili halikubaliki wala halipaswi kuungwa mkono na Mtanzania yeyote yule mwenye akili timamu na anayethamini Umoja wetu wa kitaifa.
Pia nimesikitishwa na kuumizwa zaidi, kuna Watanzania wenzetu wanalichukulia jambo hili katika mizaa na kuchochea nia ovu ya kutaka kuligawa taifa. Wapo waliotoa matusi ya nguoni kwa Mh. Rais, matusi yasiyokuwa na staha wala heshima na si maadili yetu ya kitanzania , huku wakimuhusisha na tukio hilo jambo ambalo sio kweli na wala halipaswi kuaminiwa na mtanzania hata mmoja. Moja ya watu hao yupo Mange Kimambi, binti wa kitanzania ambaye jana aliporomosha matusi ambayo si kawaida kwetu kuyasikia wakitukanwa viongozi wetu wa nchi jambo ambalo halikubaliki.
Katika muktadha huo huo wa mazaa na matusi yasiyo na maadaili, kuna kijana mwingine Suleiman Othman ambae ameandika mambo ya hovyo kabisa katika ukurasa wake wa facebook, kushabikia shambulio hilo alilofanyiwa Mh. Lisu nalo ni la kupuuzwa na mtu huyo asakwe kwa nguvu zetu zote mpaka akamatwe ili aisaidie serikali kupata majibu sahihi ya maswali kuhusu shambulio hilo. Watu wa namna hii hatujawazoea katika jamii yetu na hatuhitaji kuwa na watu wasio na heshima kama hawa.
Watu kama hawa wanaweza kuliingiza taifa letu katika machafuko mchana kweupe kabisa kama wataachwa waendelee na tabia zao za hovyo. Tabia zao hizi zinapotosha watanzania kwa kiwango kikubwa sana jambo ambalo litatuondoa katika AGENDA ya msingi na kutuingiza kubaya. Tumekuwa na umoja wa kitaifa wenye nguvu ambao ndio msingi wa Amani yetu siku zote.
Ndugu zangu watanzania lazima tukumbuke tuko katika vita na watu wenye maslahi mapana na rasilimali zetu. Wapo watanzania wenzetu ambao walishaunda mtandao wao mkubwa wa kujimilikisha na Kula wapendavyo rasilimali za nchi yetu. Watu hawa hawawezi kukaa kimya hata kidogo. Watafanya waliwezalo hata kama kwa kupandikiza chuki za udini au siasa au kijamii kwa gharqma yoyote, ili tu tusiwe na umoja wa kitaifa na kurudisha nchi yetu katika mikono yetu.
Nia Ovu yoyote au mipango yeyote inayosukwa yenye dhamira ya kuzifanya siasa za nchi yetu Tanzania ziwe za kiuhasama tuzikatae kabisa. Hatujawahi kama nchi kuwa na siasa za uahasama au uadui wa kuuwana mchana kweupe kama wanavyotaka kutuaminisha watanzania. Kwa vyovyote vile waliofanya tukio hilo wana lengo la kutugawa na kupandikiza chuki za machafuko katika jamii za kitanzania. Katika hili watanzania tuwe makini sana.
Mambo haya ya kupandikiza matukio ili kuleta taswira fulani katika nchi sio mageni hapa duniani, ingawa kwa Tanzania hatujawahi kuwa nayo. Mambo haya yanatokea hata kwenye mataifa makubwa likiwemo Marekani, Uingereza, Urusi na nchi za ARABUNI zilifarakanishwa na kuingia katika machafuko ya wao kwa wao kwa kupandikiziwa matukio ya namna hii. Mkumbuke tunayo Gesi, Tunayo Madini, Tunayo Mafuta, Tunayo URANIUM, Tunao wanyama katika mbuga zaidi ya 5 nchini, hizi zote ni biashara zinazowindwa na dunia nzima na wakiwemo watanzania wachache wenye Ulafi wa kula peke yao rasilimali za nchi na wengine tukiendelea kuwa masikini.
Katika kudumisha umoja wa kitaifa tushirikiane kuwasaka kikundi hiki kiovu kinachotaka kutuharibia nchi yetu kwa kuwa maslahi yao yamenyang'anywa au kuzuiliwa kwa njia moja au nyingine. Hata kama watakuwa wanaongozwa na mataifa makubwa ya nje umoja wetu nguvu kubwa kuliko wao.
Rais ana uadui na mafisadi tu na waliojilimbikizia mali za nchi yetu kwa ajili ya familia zao. Hawa wataendelea kupandikiza matukio ya namna hii lakini tukiwa na umoja wetu hakuna litakalotushinda kama taifa. Walianza na Kibiti serikali imewadhibiti na sasa wamehamia upande wa pili yote haya ni kupandikiza chuki na kuleta hisia mbaya katika jamii zetu.
Nawatakia ASUBUHI NJEMA NA IJUMAA NJEMA
UMOJA WETU NDIO USHINDI WETU.
Joseph yona
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: