Mabasi saba ya abiria yamekamatwa na kutozwa faini kwa kosa la
mwendokasi na kutofuata sheria za usalama barabarani huku wakihatarisha
maisha ya abiria.
Kamatakamata hiyo ambayo imesimamiwa na Kamanda wa kikosi cha usalama
barabarani Fotunatus Muslim akiwa na timu ya viongozi na askari mkoa
wa Morogoro imefanyika usiku wa kuamkia leo.
Zoezi la ukamataji mabasi hayo limefanyika eneo la Dumila Wilaya ya
Kilosa mkoani hapa, zoezi lilichukua takribani masaa mawili ambapo
mabasi hayo yamezuiwa kuondoka mpaka asubuhi huku yakitozwa faini.
Kamanda Muslim amesema jeshi hilo halitakubali kuona maisha ya watanzania yakipotea kutokana na uzembe wa baadhi ya madereva.
Amesema kikosi hicho cha usalama barabarani kimeahidi kupambana na
madereva wa mabasi ya abiria hasa nyakati za usiku kwani ndio wamekuwa
wakiendesha kwa mwendokasi huku wakidai serikali muda huo inakuwa
imelala.
Mabasi ya abiria zaidi ya saba yanayofanya safari kati ya mkoa wa Mara
(Musoma) Dar es salaam, na Mwanza- Dar es salaam yamekaguliwa na kutozwa
faini.
Muslim amesema madereva wengi wamekuwa wakifuata sheria za barabarani
nyakati za mchana kwa kuhofia kukamatwa kutokana na tochi zilizopo na
inapofika nyakati za usiku madereva hao wamekuwa wakitumia mwanya wa
kuendesha kwa mwendo kasi.
Akizungumzia dhamira ya Polisi Muslim amesema ni kuwalinda raia na mali
zao na kuwataka askari wa usalama barabarani kuacha kufanya kazi kwa
mazoea.
Amesema doria ni endelevu na sasa itakuwa kwa nchi nzima kwa usiku na
mchana huku akiwataka madereva hao kuacha kudanganyika kwa madai kuwa
tochi usiku hazifanyi kazi usiku na kwamba tochi sasa zitakamata mpaka
usiku.
"Nimekuja na slogani ya Kamata hii ni kwa wale madereva wasiotii na
kufuata sheria na tutapambana nao kila wakati na nyakati zote na hiyo
itasaidia abiria kusafiri salama na matumizi ya barabarani kuwa bora,"
amesema kamanda Muslim.
Mmoja wa abiria aliyejitambulisha kwa jina la Leon Mwete aliyekuwa
katika moja ya basi yaliyokamatwa eneo hilo la Dumila amesema zoezi hilo
ni zuri na linafaa kuendelea.
Amesema hii itapunguza ajali za barabarani na kwamba kwa sasa uendeshaji wa madereva wengi ni mzuri ukilinganisha na zamani.
Naye kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro Boniface
Mbao ameeleza kuwa yeye akiwa msimamizi mkuu ataendelea kusimamia na
kufanya oparesheni za usiku na mchana kama maelekezo yaliyotolewa
0 comments: