Mwenyekiti
wa Chama cha demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe amefunguka na
kujibu hoja za kwa nini mpaka sasa CHADEMA hawajafungua kesi kutokana na
shambulio Tundu Lissu ambapo amesema ni kutokana na kuwa kipaumbele
chao cha kwanza ni kuokoa maisha ya Lissu.
Mh.
Mbowe ameyasema hayo wakati akizungumza jana na wanahabari ambapo
amesema kuwa baada ya tukio la Lissu kutokea akili na mawazo ya Chadema
yalikuwa kwenye kuokoa maisha ya Lissu na wanasubiri mambo yakiwa sawa
wataangalia kufanya lolote linalowezekana kwan wakati huo.
"Kwa
nini Chadema hatujafungua kesi? Kesi unafungua kwa nani? Anayechunguza
ni nani? Chadema tumeshafungua kesi nyingi ya akiwepo Ben Saanane
msaidizi wangu aliye[potea kusikojulikana, Kesi ya nyani unapeleka kwa
Tumbili. Priority yetu sisi ni kumuokoa Lissu na siyo Kesi. Kupigania
maisha yake ndicho kitu tuliona kinachofaa kufanywa na ndicho
tunachofanya mpaka sasa", amesema.
"Ninaamini
tu mambo yakikaa sawa vichwa vyote hivi vya Chadema vitajua kama
tunaweza kufungua kesi au kitu gani kingine ambacho kinafaa kufanywa
endapo tu afya ya Mh. Lissu ikishaimarika" ameongeza
Akizungumzia
kwanini mpaka leo dereva wa Lissu hajarudi nchini ili kwenda kuripoti
polisi kama jinsi jeshi la polisi lilivyoagiza, Mbowe amesema kwamba
kijana huyo atarudishwa nchini pindi tuu wataalamu wa afya wanaomhudumia
wakitoa ripoti afya yake kama iko salama na wao hawapo kwa ajili ya
kumficha.
"Wiki
iliopita nilisema dereva wa Mh. Lissu yupo Nairiobi kwa ajili ya
matibabu ya kisaikolojia. Hatukuona kama ni busara kumtelekeza wakati
alikuwepo kwenye matatizo na boss wake. Madaktari wakituthibitishia kuwa
yuko timamu atarudi nchini kwani hatuko kwa ajili ya kumficha mtu. Yule
kijana ni kama mtoto wa Lissu, dereva na mlinzi wake, wana miaka mingi
pamoja tangu Lissu anagombea ubunge kwa mara ya kwanza" amesisitiza.
Ameongeza
pia dereva atakuja kuzungumza nini kilitokea na yeye alijiokoaje
naamini aliyekuwa anashambulia alikuwa hajalenga kumuacha hai mtu hata
mmoja hivyo mimi siyo msemaji sana wa dereva wake Lissu lakini akipona
ataelezea mwenyewe kila kitu.
0 comments: