Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Bongo Fleva nchini Ali Kiba amesema
moja ya mafanikio anayojivunia nayo katika kazi ya muziki kwa mwaka huu
ni ushiriki wake tena katika onyesho la Coke Studio msimu wa mwaka huu.
Ali Kiba ambaye amefanya kolabo kwa kushirikiana na mwanamuziki nguli
kutoka Nigeria, Patoranking, amesema katika mahojiano hivi karibuni kuwa
anajivunia kuwa miongoni mwa wanamuziki wanaoshiriki kwenye msimu wa
tano wa Coke Studio unaoendela ambapo kwa hapa nchini onyesho lake
linarushwa na runinga ya Clouds kila Jumamosi saa 12 jioni.
Anasema ushiriki wake kwa mara ya moja ya kwenye mafanikio kwani rekodi
yake imezidi kuongezeka katika anga la kimataifa na ameweza kujiongezea
washabiki ambao wanafuatilia shindano hili kupitia luninga,vyombo vya
habari na mitandao ya kijamii.
Mbali na kuongelea mafanikio ya kupata washabiki amesema kuwa amefurahi
kufanya kolabo na msanii wa nje ya nchi kwa kuwa ameweza kujifunza mengi
kupitia ushiriki wake kwenye Coke Studio.
“Jambo lingine ambalo naliona ni kubwa kama msanii ni kukubalika kufanya
kazi na kampuni kubwa kama Coca Cola kazi hii imenifanya nizidi
kujiongezea mashabiki na umaarufu wangu kuongezeka”Alisema.
Alisema onyesho la Coke Studio linadhihirisha kuwa muziki wa Bongo Fleva
unazidi kukua na kuwa maarufu sehemu mbalimbali barani Afrika kutokana
na jinsi linavyofuatiliwa na idadi kubwa ya watu hususani vijana.
Aliwataka wanamuziki wachanga wanaochipukia kufanya kazi kwa bidii ili
kuhakikisha wanapata mafanikio na kuongeza kuwa mafanikio yanapatikana
kwa kufanya kazi na makampuni makubwa ya biashara mojawapo ikiwa ni
kushiriki kwenye maonyesho makubwa kama haya.
“Fani ya muziki inazidi kukua kiasi kwamba wakati wa kufanya muziki wa
ndani tu imekwisha na inabidi kuvuka mipaka na kolabo kama hizi za Coke
Studio zinasaidia kupata uzoefu na kufungua milango ya
mafanikio”.Alisema.
Alimalizia kwa kuwapongeza wanamuziki wenzake kutoka Tanzania ambao yuko
nao katika msimu wa Coke Studio mwaka huu.Wanamuziki hao ni , Rayvanny,
Izzo Bizness, na Nandy.
0 comments: