VITA YA UCHUMI YALETA MITIZAMO TOFAUTI TANZANIA

*VITA YA KIUCHUMI YASHIKA KASI TANZANIA*

                                Anaandika _Jerry C. Muro_

Tangu kuanza kwa Sakata la *MAKINIKIA,* Almasi na Tanzanite, tumeshuhudia *MWINGILIANO* wa matukio Makubwa kwa taifa letu, Moja kubwa ni jitihada za *Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli* katika kurejesha *RASILIMALI* za Tanzania kwenye *HIMAYA* ya taifa ameanza vita ngumu ya *KIUCHUMI* kuwahi kutokea Duniani, vita ambayo mwisho wa siku *HUIBUA* vita halisi ya kupigana *RISASI na MABOMU,* Rejea Kilichomuua Rais wa Libya Mohammed Gaddafi.

Ujio wa Matukio Ya watu kujeruhiwa kwa Kupigwa Risasi, na Taifa kujeruhiwa na Wanasaiasa wasio *WAZALENDO* ambao wameingia mikataba Aidha kwa kujua au kwa kutokujua *IMETUFIKISHA* hapa tulipofika, Najaribu kutafakari *TUENDAKO* napaona pazuri lakini ili tufike lazima *KUJITOA MHANGA*, Mhe *Rais, Dkt. John Pombe Magufuli* ameanzisha mapambano ambayo anajua mwisho wake *HUENDA* akauwawa yeye au taifa likakombolewa *KIUCHUMI* Haya Mambo mawili nataka Leo bila woga niseme *YANAWEZA KUTOKEA,* kama sio sasa basi miaka Michache ijayo.

Wanatanzania tulioa nchini tunaungana na *Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli* kwa kumsaidia kupigana vita hii na tunaomsaidia tuko watu wa Aina mbili :-

1. Wananchi ambao wamekubali kuonyesha *UZALENDO* wao kwa kutoangalia kilichotokea *NYUMA* na kukubali kuanza mapambano kuanzia mahali tulipo sasa na kwenda mbele hawa wanamsaidia *Rais, Dkt. John Pombe Magufuli* KIKAMILIFU hapa niko mimi (Jerry C. Muro)

2. Wananchi wanaomsaidia Mhe Rais, *Dkt. John Pombe Magufuli*!kwa kumvuta shati na kumwambia kabla hujaingia *VITANI* Tazama uku nyuma kwanza, kuna mikataba ambayo watangulizi wako waliingia hata kama mikataba ni mibaya kwanza unapaswa kutazama uku kwanza kabla haujaingia *VITANI,* Hawa ndio kina (Tundu Lissu na wenzake haswa Upinzani) hawa wanamsaidia *Rais, Dkt. John Pombe Magufuli* vizuri tu ila usaidizi wao *UNATAKA* kuleta vita ingine ya ndani vita ya wenyewe kwa wenyewe mana unaposema Tazama kwanza nyuma uku, Tazama mikataba hii ya zamani, unataka *Mhe Rais Magufuli* aanze kumkamata Mhe Mwinyi, Mhe mkapa, Mhe Kikwete, sio hao tu aanze kuwakamata mawaziri na Wabunge wote waliokuwepo enzi zile, hapa tutaanza vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo *Mhe Rais, Dkt. John Pombe* Magufuli *AMESHAIONA* na ameamua kuikwepa, mana viongozi wengi wa zamani wako *CCM na UKAWA* Tazama baadhi ya mawaziri wakuu wastaafu wengine wako Ccm, wengine wako ukawa nyinyi mnawajua vizuri WAPO, au mmemsahau Mzee EDWIN MTEI alikuwa Nani enzi zile za nyerere nchini, ndio mana nasema katika kundi hili wanaanza tukianza vita ya wenyewe kwa wenyewe wanadhani na wao wataweza kuiangusha Ccm madarakani wakatawala kirahisi? Mtatawalaje wakati kuna vita, tutafanyaje uchaguzi wakati tunakimbia nchi na kuwa wakimbizi Burundi na Rwanda tena kama wao walivyo kuwa kwetu zamani, hivi mnadhani hao Marais, mawaziri na Wabunge wa zamani waliopitisha na kuingia hiyo mikataba ambayo mnataka magafuli aanze kuitazama kwanza kabla hajaijgia VITANI hawana Familia zao, ndugu jamaa na watu walionufaika wakati wakiwa madarakani kama unabisha Jaribu kutembelea Instagram, Twitter na Facebook account ya MTOTO WA RAIS MSTAAFU uone anavyopambana ndio mtanielewa hapa nachosema, kwani mnadhani yeye hachafuki au Haya Mambo hayamuumi roho au kwakuwa ni *MKWERE* Mwenye roho ya *MKURYA* ndio mnamuona *HIVYO.*

Niwakumbushe Mhe Magufuli aliposema *HATAKI*!kufukua makaburi ya zamani mana huenda tukashindwa *KUFUKIA* hamkumwelewa? Kama mlimwelewa nadhani hawa watu wa kundi la pili wanapaswa *KUELIMISHWA, KUKUMBUSHWA* vizuri japo safari hii wanaelimishwa na *KUKUMBUSHWA* kwa *LAZIMA* na *UKALI.*
Tukirudi kwenye utaratibu wa kutazama nyuma kamwe *HATUTAPIGA* hatua mbele, mana Tunajua, na kutambua kuna makosa yalifanywa na ndio mana Juzi Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai *ALITUBU* na kuungama kwa niaba ya WOTE waliohusika, ndugu zangu Ukiona *SPIKA* wa Bunge anathubutu *KUTUBU, KUUNGAMA* hadharani tena akiwa *LIVE* kwenye vyombo vyote vya Habari nilidhani *INGETOSHA* kwa watanzania kuja pamoja na *KUSAHAU* hili neno *MIKATABA* ya zamani, na kuwaomba *WAJUVI* wa masuala ya Sheria akiwemo kaka yangu *TUNDU LISSU* kutumia *AKILI ZAO KUBWA* kutunasua hapa tulipokwama, au tulitaka Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli amuite Mmoja Mmoja kwenye TV na radio kuwa Njoo tusaidie? Hapana hawezi kufanya hivyo tunachotakiwa ni sisi wenyewe kwenye maeneo yetu tuliyopo tumuunge mkono moja kwa moja *TUSONGE MBELE.*
Kama watu wanatumia *AKILI ZAO KUBWA* kutuvuruga Kwanini wasitumie *AKILI ZAO KUBWA* kutukwamua hapa? Kwani wao sio watanzania? Au wanataka *KUTUSAIDIA KUTUKWAMUA* wakiwa *MADARAKANI* na wao?

*KWENU WATANZANIA WALIO NJE YA NCHI.*
Kuna baadhi ya watanzania Kwa makusudi kwa kujua au kutojua WAMEAMUA kutukwamisha, Kazi yao ni kukosoa tu pasipo kujua Mhe Job Ndugai alishafanya TOBA kwa yaliyotokea, niwaambie tu TAIFA Lina huitaji MKUBWA wa kutoka hapa tulipo, tusifungwe na Hadithi za Kina WALTER RODNEY how uerope underdeveloped Africa? Kwa kuanza kuangalia MIKATABA ya zamani, *TUANGALIE RASILIMALI *zetu kwanza *MIKATABA* sio vitabu vitakatifu (Bible au Quran tukufu) useme *HAIBADILIKI* au kuvunja, kwanza sisi kwetu Wakristo utaona mabadiliko makubwa kabisa kwenye Bible tunayo inaitwa (KJ) Yaani King James Version ndio itakuwa hii MIKATABA ya kina *MANG'UNG'O* wa *USAMBARA*.

Mwisho nimjibu tu Mtanzania mwenzangu ambae yuko uko *UGHAIBUNI* uko, sitaki kumjibu yule Mtani wangu *(MPARE)* Hapana, Leo namjibu Kaka yangu *CHAHALI* ambae ameweka mikataba, vibali vya kuhalakisha Utoroshaji wa MADINI ya Almasi (Dimond) akijaribu kutupia lawana serikali, Brother unapotea sana nadhani huenda ni frastruation za Maisha na Umeona uzee umeingia na huna cha kufanya uko na ukirudi uku Mambo mazito, sasa sikikiza kaka yangu:-

"Unasema serikali inatuhadaa wakati yenyewe ndio imetoa hio document na kibali! Provisional sum kwa mujibu wa ukokotoaji ilipaswa kua *usd 29 mill* sio *usd 14 mil*!na Kwa hio actual tunaitegemea iwe around that figure kwa vile basis ya provisional ni prevailing world market prices, unanielewa Mpaka Hapa kaka?

Sasa Kwa vile provisional tutakayoenda nayo Belgium ni *USD 14*!maana wanunuzi watakuuliza una mzigo kiasi gani umeleta mnadani na ungependa kupata bei gani unategemea final itakua 29  wakati wewe umesema mbuzi wako thamani yake ni 14?tuko Sawa sawa kaka?

Leo nataka kukuonyesha kitu kidogo hapa watanzania nataka waone tofauti ya tui la nazi  *(CHAHALI)*na Maziwa (muro) ilivyo, huenda tui la nazi na Maziwa rangi zikafanana lakini ladha tofauti, ila kila kimoja kina umuhimu wake kwenye mapishi, pwani wanapenda nazi sana na machame kaskazini tunapenda Maziwa.

Pili wakati wewe hauko kule unategemea yeye akuambie kwamba aliuza kwa bei fulani? Ndio maana moja ya pendekezo nao waende kwenye mnada kujihakikishia! Issue hapa ni kwamba wathaminishaji wa serikali wameunder *VALUE* ili mwenye mgodi apate faida kubwa na alipe kodi na mrahaba mdogo! Hizo kodi na mrahaba zinakua calculated on export values ndio hio provisional *VALUE,* unaelewa kaka yangu wa *UGHAIBUNI?*

Ni sawasawa na bandarini mzigo ukifika wewe hata ukisema gari vogue umenunua dola elf kumi TRA wanafanya uthamini upya wakiona risiti zako za uongo wana uplift na unalipa kodi kubwa upya lakini ukiwahonga wakakubaliana na thamani ndogo ukalipa wakati wa kuitoa Pccb wakikukamata kwamba ushuru umelipa kidogo utasema mbona serikali ilitathmini? Itabidi ulipe difference!

Kwa hio kilichokamatisha ni hizo hizo risiti walipoona hizo kilo na thamani wakatilia shaka wakasema vipimwe upya matokeo ndio hio *thamani ya 29.* Kwa hio wathamini wa serikali wamekamatwa kujua ilikuaje wakatoa thamani ndogo kuliko wenzao? Je walishawishiwa na mwenye mgodi? Kama walishirikiana basi mali *ITATAIFISHWA.*

Ndugu zangu sikupenda kwenda uko kwenye mambo makubwa nikasahau kuwa nina watani zangu wapare ambao wengi hawapendi kusoma mambo marefu sana kama Haya, lakini katika zama hizi, lazima tusome sana tupate maarifa ili tusipotoshwe.

Get well soon kaka yangu Tundu antipasi Lissu, Nakutakia afuheni, jua sisi bado tupo Tunapambana, tunakusubiria kwa hamu urudi, mana tukio lako Lina maswali mengi kuliko majibu, *UGUA POLE KAMANDA LISSU.*

*Mwandishi wa Makala hii, ni Mwanahabari mwandamizi za Uchunguzi kwa Kipaji (talented), Mtaalamu wa Uongozi wa Biashara na Masoko (kitaaluma) Mwenye Shahada ya Uzamili (Master Degree) MBA (2015)
Email :jerrymuro98@gmail.com
Tel Mob 0785333999
Instagram page @jerrymuro1980
Share on Google Plus

0 comments: