WAZIRI MWAKYEMBE AUDHURIA TAMASHA LA JAMAFEST NCHINI UGANDA
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe
akipokelewa na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda Bi. Asha
Abdalla Mwelekwa mara baada ya kufika katika ofisi hizo ili kuonana na
Kaimu Balozi ambaye ni Naibu Balozi Elibariki Nderimo Maleko.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe
akaisaini kitabu cha wageni katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania Nchini
Uganda mara baada ya kufika ofisini hapo, pembeni ni Kaimu Balozi ambaye
ni Naibu Balozi nchini Uganda Balozi Elibariki Nderimo Maleko.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe alifanya
mazungumzo na wajumbe wa kamati ndogo ya maandalizi ya Tanzania ya
Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST)
mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya Tamasha hilo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe
akiangalia ngoma ya Utamaduni ya Kikundi cha Taifa cha Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar wakati alipofika katika uwanja wa Uhuru Kololo
kuangalia maonesho ya bidhaa za wasanii wa nchi mbalimbali Wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe.
Mwakyembe akiangalia bidhaa za wasanii mbalimbali wa Tanzania alipofika
katika Uwanja wa Uhuru Kololo na aliwapongeza Watanzania hao kwa
kuitikia wito wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Joseph Magufuli kwa kutekeleza sera ya Viwanda kwa kuonesha uwezo
walionao wa kutengeneza bidhaa mbalimbali zenye ubora kwa malighafi
zinayopatikana nchini, aidha aliahidi kwamba wakati wa Bunge la Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania litapokaa katika kikao chake cha mwezi wa
Novemba 2017 wasanii ambao walishiriki maonesho ya bidhaa za sanaa
Kampala wataalikwa Dodoma kwa ajili ya kufanya maonesho kama hayo ili
kuonesha ubunifu wa Watanzania waliona juu ya kuzalisha bidhaa za sanaa.
Mhe. Mwakyembe akipokea bidhaa ya sanaa ya ubunifu ya hot pot la kuwekea chakula wakati alipotembelea banda la Nchi ya Burundi.
Mhe. Mwakyembe akiangnalia bidhaa za viatu vinavyozalishwa na wasanii
wa Nchi ya Rwanda ambvyo vikanyagio vyake vimetengenezwa kwa matairi ya
gari wakati alipotembelea banda la nchi hiyo.
Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mwakyembe akitembelea banda na nchi ya Kenya na kuangalia bidhaa za nchi hiyo.
Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mwakyembe akitetembelea banda na nchi ya Uganda na kuangalia bidhaa za nchi hiyo.
Ubalozi
wa Tanzania Nchini Uganda pamoja na Watanzania wanaishi nchini humo
wamepongezwa kwa hatua walizozichukuwa za kuungana na serikali yao ya
kuhakikisha kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inafanikiwa kushiriki
katika Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki
(JAMAFEST) linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Uhuru Kololo jijini
Kampala nchini Uganda.
Waziri
wa Habari utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
alitoa pongezi jana katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Uganda
alipofika kuonana na Kaimu Balozi ambaye pia Naibu Balozi wa Tanzania
Nchini Uganda Elibariki Nderimo Maleko na kupokea taarifa ya maandalizi
yaliyofikiwa ya JAMAFEST kwa upande ushiriki wa Tanzania.
Mhe.
Mwakyembe alisema Ubalozi wa Tanzania Nchini Uganda chini ya Naibu
Balozi Maleko na Watanzania wanaoishi Uganda chini ya Mwenyekiti wa
Umoja wa Watanzania wanaoishi Uganda (UTU) Benjamini Lesile walionesha
mfano bora wa kujali nchi yao kwa kuwashajihisha wafanyabiashara pamoja
na Watanzania wanaoishi Uganda kutoa michango yao ambayo imeweza
kufanikiwa vizuri na kuwezesha Tanzania kushiriki JAMAFEST kwa ufanisi
na kwa faida ya nchi yao.
Watanzania
wanaoishi nchi Uganda kwa kushirikiana na Kampuni ya Hariss
International LTD ya Mfanyabiashara Mtanzania waliweza kutoa michango
yao ambayo ilisaidia pale nchi iliyoandaa maonesho ilishindwa
kuwawezesha washiriki kama vile maji ya kunya na vinywaji baridi, mahema
na usafiri ambapo zaidi ya katuni za maji na soda mia mbili pamoja na
mahema vilitolewa na Watanzania hao, kwa hiyo aliwasisitiza Watanzania
walio ahidi kuchangia kutoa michango yao kwa mujibu wa ahadi walizotoa.
"Ninamshukuru Balozi Maleko, Kampuni ya Hariss International LTD ,
Mwenyekiti wa UTU Benjamin na Watanzania wanaoishi Nchini Uganda kwa
uzalendo wao" alisisitiza.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Bara Mhe. Mwakyembe
aidha ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua
iliyochukuwa ya kipekee ya kushiriki JAMAFEST kwa kuvishirikisha vikundi
vya Utamaduni na Sanaa vya taifa ambavyo vilitia fora katika maonesho
kwa kuonesha utamaduni wa Visiwani, kwa hiyo alisema kwamba katika
matamasha yajayo vikundi vya Utamaduni na sanaa vya taifa vya Tanzania
Bara vitashirikishwa. Zanzibar iliwakilishwa na kikundi cha Taarabu cha
Taifa na kikundi cha sanaa cha ngoma cha Taifa.
Mwaka
huu jumla ya Wasanii wa utamaduni na sanaa za ubunifu wa Tanzania
wapatao 196 walishiriki Tamasha hilo kwa kuonesha bidhaa zao za ubunifu
za Ngoma, Mavazi, nguo, wasarifu wa milango na makasha ya mbao, vyakula
na Lugha ya Kiswahili.
Tamasha
la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) lengo
lake ni kutafuta soko la bidhaa za ubunifu za utamaduni na sanaa sio tu
katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki bali hata sehemu
nyingine za dunia kwani ni bidhaa zinazobeba zaidi soko katika sekta ya
utalii ambazo zimekuwa zinalishwa kwa wingi katika nchi wanachama na
kukosa soko. Tamasha hilo linafungwa leo Alhamis jioni.
0 comments: