Thursday, October 5, 2017
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondini, Ally Hapi amesema atawafutia leseni wamiliki wa
hoteli na kampuni binafsi ambao hawajatoa mikataba ya ajira kwa
wafanyakazi wao.
Aliwabana
wamiliki hao jana alipokuwa katika ziara wilayani humo na kutembelea
baadhi ya hoteli na kampuni binafsi kwa lengo la kuzungumza na
wafanyakazi.
Awali, wafanyakazi walilalamikia mazingira magumu ya kazi ikiwamo mishahara duni na kufanya kazi bila mikataba.
Mmoja
kati ya wafanyakazi 23 wa Hoteli ya Tangren iliyopo Mikocheni, Lilian
Semtanda alisema licha ya kufanya kazi kwa miaka mitano, hajapatiwa
mkataba huku akinyimwa stahiki ikiwamo likizo na matibabu.
0 comments: