Na Joseph Yona
kutokana na hoja iliyo letwa na katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi Taifa ndg Humfrey Polepole imeibua hisia tofauti tofauti za Wantazania na kuwaacha wakiwa wamegawanyika katika amafungu na hii ni kutokana na watu kukosa uelewa kuhusu neno UKATIBA
Labda nianze kwa kutoa maana ya UKATIBA kwani ndio limeibuka na kuleta hoja za sintofahamu kwamba neno lenyewe halipo katika kamusi lakini tufahamu chimbuko la lugha yetu na tujue kwamba kiswahili chetu kinazidi kutanuka
UKUTIBA ni neno la msimu na asili ya neno la msimu huja na kupotea lakini linaweza baki na kuingizwa katika kamusi kama neno hilo linaweza kuwa na muenelezo wa matumizi neno hilo likiwa limebeba dhana kubwa ya kufikisha ujumbe ulio kusudiwa sasa
UKATIBA inaeleza umiliki wadhana zima ya KATIBA kwa tafsiri yake ni kwamba UKATIBA ni kitendo cha kuyafanya na yale yote yaliyomo ndani ya katiba kwa kufwata misingi na taratibu zote zilizopo ndani ya katiba
Ndg Polepole alisema kuwa kutokana na takwimu za TWAWEZA Watanzania wengi wanapenda wanavutwa kuona UKATIBA kwenye nchi yetu zaidi kuliko KATIBA kwa sababu kitu chenye maana kwa hapa Tanzania na Nchi yeyote ni UKATIBA na si KATIBA
sababu ukatiba unatoa majumuhisho ya jinsi gani tuishi na viongozo wetu ni mambo wanapaswa wayafanye kwetu sisi Watanzania
Mwenezi alisema na aliwataka Viongozi wa CCM na Serikali kuishi UKATIBA kwani unaweza kuwa na katiba nzuri yenye kusomeka vizuri na kueleweka na mataifa mengi lakini isiwe na tija kwa taifa na watu wa hali ya chini ambao kiu yao ni kuona maendeleo kwenye maisha yao ya kila siku na sifa kubwa kwa taifa kuwa na katiba nzuri
Kutokana na tafsri hiyo tunaweza tumia nguvu kubwa akili nyingi na gharama kubwa katika uwekezaji kwenye KATIBA lakini isiwe na faida kwa Taifa maana tumeweza kushuhudia mataifa yaliyofanikiwa kwa kuweka UKATIBA mbele kama China Kolea USA na pia tunawaona wenzetu kenya wanavyo pata tabu kwa kuweka katiba mbele
Tume pita katika vipindi vinne vya uongozi lakini kipindi hiki au awamu hii Rais JPM amweza fanikiwa kuwaongoza watendaji wake kuishi katika UKATIBA na bado anaendelea utaona mabadiliko mengi sana yametokea kama uwajibikaji na uzarendo tunaona Taifa linasonga mbele
Watanzania wote ni wakati wetu wa kuishi UKATIBA halfu KATIBA itafwata nyuma yetu tuweke maslai yetu binafsi nyuma halfu taifa mbele tuachane na ubinfsi tuachane natamaa
ikumbukwe na ifahamike kuwa hakuna atakae toka nje ya taifa letu na kuja kutuletea maendeleo ndani ya Taifa letu hivyo Watanzani tukubali kuishi UKATIBA ili tusonge mbele
napia tuifahamu dhana ya Polepole ni kulileta Taifa pamoja na kuleta mshikamano na kumtia nguvu Rais wetu kwani amekuwa mstari wa mbele katika kuishi UKATIBA
NI
JOSEPH YONA
Mwenyekiti wa ccm tawi la bokorani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: