Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe amepongeza kitendo cha Rais John Magufuli
kuitenganisha Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwa kwa zaidi ya miaka
saba kambi hiyo ilikuwa inaishauri Serikali kufanya hivyo.
Mbowe
amesema hayo jana Jumamosi kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul,
baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata
ya Dareda.
Alisema
kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge zinaonyesha kuwa kambi rasmi ya
upinzani ilikuwa inashauri wizara hiyo itenganishwe lakini ushauri wao
haukufanyiwa kazi.
"Wizara
ya Nishati na Madini ni wizara nyeti mno na mara nyingi tumekuwa
tukiishauri Serikali iitenganishe wizara hiyo kwani ni kubwa na nyeti
ila sasa wameona ushauri wetu unafaa na kuzitenganisha," alisema Mbowe.
Alisema
suala siyo nani anafaa kuwa waziri na nani hafai kuwa waziri au ukubwa
wa wizara ila suala ni kuona namna gani ya kuendesha Serikali ya Awamu
ya Tano.
"Magufuli
ajitafakari namna anavyoendesha Serikali kwani matakwa ya viongozi
ndiyo yanakuwa maelekezo ya kuendesha nchi na hata mawaziri wanafanya
kazi kwa matakwa ya mtu," alisema Mbowe.
0 comments: