Sunday, October 8, 2017
Kwenye
ukurasa wake wa Facebook Zitto Kabwe ameandika ujumbe akiwapongeza
Mawaziri hao walioteuliwa ambao wengi wao ni vijana, huku akiwataka
kuchapa kazi kwa bidii.
“Uteuzi
wa vijana kushika nafasi za juu ni hatua nzuri, naona vijana wengi
wamepewa majukumu makubwa, ninawaombea watekeleze majukumu kwa weledi
mkubwa”, ameandika Zitto Kabwe.
Jana
Rais Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuongeza
wizara mpya mbili, baada ya kuzivunja baadhi ya wizara ambazo zilikuwa
na vitengo vingi.
0 comments: