Mbunge
wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye amepigilia msumari kauli iliyotolewa
na Spika wa zamani wa Bunge , Pius Msekwa kuhusu miaka ya uongozi na
kusema misimamo hiyo ndiyo misimamo ya Chama Cha Mapinduzi chini ya
Mwalimu Julius Nyerere.
Nape
Nnauye ameweka video ya Pius Msekwa akielezea juu ya ukomo wa kiongozi
madarakani na kusema chama hicho kilishafikiria miaka ya nyuma kuongeza
miaka kutoka 10 na kuendelea lakini waliona miaka kumi inatosha kwa mtu
kuongoza na kusisitiza ikiwa miaka 15 ikatokea mkapata kiongozi mbaya
miaka hiyo itakuwa ni mingi sana.
"Miaka
15 mkipata kiongozi mbaya ni mingi sana, nashauri ibaki miaka 10 kama
kiongozi ni mbaya angalau tumvumilie kwa miaka 10 tu halafu basi ndivyo
hoja ya miaka 10 ilivyopita si kama hiyo mingine hatukufikiri
ilifikiriwa ndiyo maana naposikia kuna Mbunge mmoja anataka kupendekeza
twende kwenye miaka saba kwa vipindi viwili ninataka kumjulisha kwamba
hili si wazo jipya tulishafikiri na lilikataliwa kwa hiyo mimi na imani
CCM itaendelea kulikataa hilo, tutabaki kwenye miaka mitano tu mara
mbili basi" alisisitiza Msekwa
Kufuatia
kauli hiyo ndipo Nape Nnauye alipigiria msumari na kusema hicho ndicho
Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha Mwalimu Julius Nyerere anachokijua yeye.
Siku
za karibuni Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia alidai anataka kupeleka
hoja bungeni kuongeza muda wa utawala hadi miaka 7 badala ya miaka
mitano ya sasa.
0 comments: