Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi sare za shule kwa
wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kizumbi
na Kitangili katika manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la kukabidhi sare hizo za shule limefanyika leo Alhamis Oktoba 12,2017 katika shule ya msingi Kitangiri.
Msaada
huo wa sare za shule unatokana na kampeni iliyoanzishwa na mkuu huyo wa
wilaya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika wilaya
ya Shinyanga.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi sare hizo,Matiro alisema pamoja na serikali kuwa na
sera ya elimu bure lakini wamebaini kuwa kuna watoto ambao wanaishi
katika mazingira magumu hivyo wanahitaji msaada kutoka wadau mbalimbali.
“Tulifanya
zoezi la kugawa sare kwa wanafunzi wengine hivi karibuni,na leo ofisi
yangu kwa kushirikiana na wadau wengine likiwemo shirika la wanawake na
watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO)
nimekuja kukabidhi sare za shule kwa wanafunzi 121 wa kata ya Kitangili
na Kizumbi”,alieleza Matiro.
Matiro
aliwataka wazazi kutimiza wajibu wao wa kulea watoto badala ya
kuwatekeleza kwa bibi na babu zao na wao kukimbilia mjini huku watoto
wakiteseka na kuishi katika maisha magumu.
Kwa
upande wake Mratibu wa miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake
na watoto la Promising World For Women and Children Organization
(PWWCO),Venny Raymond alisema walifanya utafiti na kubaini kuwa kuna
wanafunzi/watoto wengi katika kata ya Kitangili na Kizumbi wanaishi
katika mazingira magumu hivyo kushirikiana na wadau wengine kutafuta
sare za shule kwa ajili ya wanafunzi hao.
“Tumebaini
kuwa watoto wengi hawaishi na wazazi wao,wengine ni yatima,lakini pia
wapo ambao wazazi wao hawana uwezo kiuchumi hali inayosababisha watoto
kushindwa hata kuhudhuria masomo yao,wakitumika kama chanzo cha mapato
katika familia zao”,alisema Raymond.
Naye
Afisa Elimu kata ya Kitangili Mahmood Ibrahim mbali na kushukuru kwa
msaada huo wa sare za shule zikiwemo kaptura,sketi na mashati na
kueleza kuwa kutokana na ugumu wa maisha wapo watoto wanashindwa kupata
chakula na wengine kukosa mavazi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza kabla ya kuanza
kugawa sare za shule kwa wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu
katika kata ya Kizumbi na Kitangili leo katika shule ya msingi
Kitangili mjini Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akiwataka akina mama kuunda vikundi vya ujasiriamali ili waweze kujiinua kiuchumi
Mratibu
wa miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la
Promising World For Women and Children Organization (PWWCO),Venny
Raymond akielezea namna walivyowapata watoto wanaoishi katika mazingira
magumu katika kata ya Kitangili na Kizumbi
Afisa Elimu kata ya Kitangili Mahmood Ibrahim akizungumza wakati wa zoezi la kugawa sare hizo za shule
Diwani
wa viti Maalum kata ya Kitangili Mariam Nyangaka (CCM) akimshukuru mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kushirikiana na wadau kusaidia
watoto wanaoishi katika mazingira magumu
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wazazi,walezi na
wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kabla ya kugawa sare za
shule kwa wanafunzi hao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akimvalisha shati mmoja wa wanafunzi hao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akishikana mkono na mwanafunzi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akivalisha sare ya shule mwanafunzi
Mwanafunzi akiwa ameshikilia sketi baada ya kuvalishwa shati na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akitafakari jambo wakati wa kugawa sare za shule
Zoezi
la kugawa sare za shule likiendelea.Wa kwanza kushoto ni Afisa
Ufuatiliaji na Tathmini wa Miradi kutoka shirika linalohusika na
wanawake na watoto la Promising World For Women and Children
Organization (PWWCO).
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kizumbi Marcelina Bwathondi akijiandaa kumpa sare ya shule mmoja wa wanafunzi hao
Wazazi na walezi wa wanafunzi wakishuhudia zoezi la ugawaji sare za shule kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.
0 comments: