Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka
na kusema kuwa anatambua kuna watu Zanzibar walikuwa wanasubiri
kuapishwa baada ya uchaguzi Mkuu 2015 lakini hatambui watu hao wameishia
wapi hivi sasa.
Rais
Magufuli amesema hayo leo alipokuwa kwenye kilele cha mbio za Mwenge
2017 shereha ambazo zimefanyika Zanzibar katika uwanja wa amani.
Rais
Magufuli amedai kuwa watu ambao watajaribu kuchezea Muungano wa
Tanzania na Zanzibar watashughilika nao kwani wao wataendelea kuupigania
Muungano huo ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Sheikh
Abeid Aman Karume.
"Najua
huku Zanzibar walikuwepo watu wamejiandaa kuapishwa, sijui wameishia
wapi, tutaendelea kuupigania Muungano wetu, na yeyote ambaye atajaribu
kuuchezea tutashughulika naye" alisisitiza Rais Magufuli
Mbali
na hilo Rais Magufuli amewataka Watanzania kiujumla kuwa wavumilivu na
hali ya uchumi wa sasa na kusema kuwa ni mapito na kuahidi kuwa mambo
yatakaa sawa muda si mrefu hata kama hayatakuwa sawa sasa anaamini kuwa
watoto na wajukuu wetu watakuja kukuta mambo yako vizuri kwani mageuzi
yoyote yale huwa yanachukua muda.
Katibu
Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alikuwa mgombea wa nafasi
ya Urais Zanzibar 2015 baada ya uchaguzi kufanyika alijitangazia matokeo
kuwa yeye ndiye mshindi wa nafasi ya Urais kabla ya Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC) kutangaza mshindi.
0 comments: