Rais
John Pombe Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili ya kikazi
mkoani Mwanza na kufungua miradi minne inayolenga kuboresha uchumi wa
nchi.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema rais ambaye atafanya ziara
kesho na kesho kutwa, ataongozana na viongozi wengine hadi katika Daraja
la Furahisha na kulizindua.
Daraja hilo limejengwa ili kurahisisha mawasiliano kati ya waenda kwa miguu na vyombo vya moto.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema baadaye rais ataelekea Nyakato wilayani Nyamagana
kufungua Kiwanda cha Sayona Drinks Limited na kuhitimisha ziara kwa siku
hiyo.
Jumanne, rais atafungua Kiwanda cha Victoria Moulders and Polybags, kilichopo Igogo jijini Mwanza.
Alisema siku hiyo hiyo, ataelekea Buhongwa kwa ajili ya kufungua Kiwanda cha Dawa cha Prince Pharmaceutical Industry.
Mkuu huyo wa Mwanza aliomba ushirikiano kutoka kwa wananchi na wadau wengine ili kufanikisha ziara ya Rais Magufuli.
“Naamini
mkoa wetu umejaaliwa amani na ulinzi wa kutosha, hivyo basi, sitarajii
kusikia ripoti yeyote ya utovu wa nidhamu,” alisema Mongella.
0 comments: