Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari
kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akimkabidhi mbegu bora
ya mahindi, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi wakati wa
uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu za mahindi, mhogo na viazi lishe
uliofanyika nje ya viwanja vya ofisi ya mkoa huo jana. Kushoto ni
Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB),
Dk.Nicholaus Nyange.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi akizungumza na waandishi
wa habari wakati wa kukabidhiwa mbegu hizo za mahindi zinazokabiliana na
ukame Wema.
Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, David Makabila
akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Isamilo kabla ya uzinduzi wa
shamba darasa la mbegu ya mahindi. Kutoka kushoto ni Mtafiti kutoka
COSTECH, Dk.Beatrice Lyimo, Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha Maruku
mkoani Kagera, Jojianas Kibula, Mtafiti Bestina Daniel na Mshauri wa
Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus
Nyange.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani
Morogoro, Ismail Ngolinda, akitoa maelezo ya jinsi ya kupanda mbegu ya
mahindi.
Wananchi wa Kijiji cha Isamilo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mkulima Hernick Elias wa Kijiji cha Isamilo akizungumzia changamoto za kilimo walizonazo
Watafiti wakifanya vipimo kabla ya uzinduzi wa shamba la mbegu za mahindi katika kijiji cha Isamilo.
Wakulima wa Kikundi cha Nguvumoja cha Kijiji cha Isamilo wakiwa shambani wakati wa uzinduzi huo.
Mkulima wa Kijiji cha Isamilo, Salome Renatus akizungumza na waandishi wa habari.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani
Morogoro, Ismail Ngolinda, akionesha namna ya ujimbaji wa mashimo kabla
ya upandaji wa mbegu za mahindi.
Ofisa Ugani wa Kijiji cha Isamilo, Issa Pegeege, akionesha jinsi ya uwekaji mbolea kabla ya kupanda mbegu ya mahindi Wema.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari
(kulia), kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akiongoza
wakulima kupanda mbegu ya mahindi kwenye shamba darasa katika Kijiji cha
Isamilo.
Mkulima wa Kijiji cha Kikundi cha Nguvu moja katika Kijiji cha Kamhanga,
Hamisi King akitoa maelekezo wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la
mahindi katika kijiji hicho.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani
Morogoro, Ismail Ngolinda, akionesha namna ya ujimbaji wa mashimo kabla
ya upandaji wa mbegu za mahindi katika Kijiji cha Isamilo.
Wakulima na wananchi wa Kikundi cha Kasimpya katika Kijiji cha Mnekezi
kilichopo Kata ya Kaseme wakisubiri maelekezo namna ya kupanda mbegu za
mahindi katika shamba darasa.
Diwani wa Kata ya Kaseme, Andrew Kalamla akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa shamba darasa hilo
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari
kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akizungumza na wananchi
wa kijiji cha Mnekezi.
Mwakilishi wa Mkoa wa Geita, Emiri Kasagala, akihutubia katika uzinduzi huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo, Robert Gabriel
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari
kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akipanda mbegu wakati wa
uzinduzi wa shamba darasa katika Kijiji cha Mnekezi. Kulia ni
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Emiri Kasagala.Picha na Dotto Mwaibale,
Geita
**
MKUU wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi amesema ataanzisha
utaratibu wa kuwapima maofisa ugani wa mkoa huo utendaji kazi wao ili
kujua uwezo wa kila mmoja wao.
Hayo ameyasema wakati Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),
ilipokuwa ikimkabidhi mbegu bora za mahindi, mihogo na viazi lishe
ikiwa ni siku yake ya kwanza kufanya kazi katika mkoa huo tangu ateuliwe
na Rais Dk.John Magufuli kushika wadhifa huo.
"Kilimo ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaingia
katika uchumi wa kati wa viwanda hivyo nitaweka utaratibu wa kuwapima
maofisa ugani wote wa mkoa huu ili niweze kujua utendaji kazi wao"
alisema Lughumbi.
Lughumbi aliwataka maofisa ugani mkoani humo kuacha kukaa maofisi kwenye
viyoyozi badala yake waende walipo wakulima kushirikiana nao kuwapa
elimu ya kilimo ili kujikomboa kiuchumi kupitia kilimo.
Mkuu huyo wa mkoa ameahidi kununua viatu vya shambani 'gambuti' na koti
na kuwa mara moja ataanza kutembelea wakulima katika maeneo yao ili
kujua changamoto zao na kusema anapenda kuona mkoa wa Geita unakuwa
namba moja kwa kilimo hapa nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa
kukabidhi mbegu hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai
wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri
serikali katika masuala yote yanayohusu Sayansi na Teknolojia na
kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na
kuhakikisha zinawafikia walengwa.
Alisema mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa
katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili
kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima
kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa na magonjwa kama batobato na ukame.
Akizungumzia mbegu bora ya viazi lishe alisema mbegu hiyo viazi vyake
vinavitamini A ya kutosha ambayo ni muhimu kwa watoto na hiyo
itawasaidia baadhi yao kuto kwenda Hospitali kuipata badala yake
wataipata kwa kula viazi hivyo.
Msangi aliwaomba maofisa ugani pale wanapokuwa na changamoto mbalimbali
za kazi yao wasisite kwenda COSTECH ili kusaidiana na kupeana mbinu
mbalimbali za kilimo.
Mkulima wa Kijiji cha Isamilo, Hermick Elias alisema kukosekana kwa
mbegu bora, wataalamu wa kilimo na kutofikiwa na pembejeo za kilimo kwa
wakati ni moja ya sababu ambayo imewarudisha nyuma katika masuala ya
kilimo lakini wanaamini kwa mbegu hizo walizoletewa na COSTECH itakuwa
nu mkombozi kwao kwa kupata chakula na ziada watauza na kujipatia fedha
za kuwasaidia.
0 comments: