Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina
ameahidi kuwa atajiuzulu nafasi yake endapo tatizo la uvuvi haramu
litaendelea kuwa sugu nchini.
Waziri Mpina ameyasema hayo jana
walipokuwa akitekeleza lundo la nyavu zinazotumika kwenye uvuvi haramu
zenye thamani ya Tsh 30 milioni zilizokamatwa mkoani Kigoma.
Mpina amesema kwamba, endapo atashindwa
kutumua dhamana aliyopewa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kukomesha
uvuvi haramu atajizulu nafasi yake. Lakini alisema kwamba, hadi kufikia
wakati huo ambao atakuwa ameamua kujiuzulu, watu wengine ambao ni
wasaidizi wake, nao watakuwa wameumia.
Serikali imepiga marufuku matumizi ya
nyavu zenye matundu madogo au uvuvi wa kutumia sumu na baruti ambao
husababisha samaki wachanga ambao bado hawajafikia wakati wa kuvuliwa
kufa jambo linaloharatisha uwepo wa samaki hao katika miaka ya mbeleni.
0 comments: