Alichokisema Mama Kanumba Baada Ya Lulu Michael Kuhukumiwa Miaka Miwili


Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na kusema kwamba leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipozikwa mwanaye ili kwenda kumzika upya.

Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo.
“Namshukuru Mwenyenzi Mungu, naishukuru Mahakama imetenda haki, naishukuru Serikali yangu awamu ya tano“

“Kalale salama mwanangu Steven Kanumba na nikitoka hapa nakwenda makaburini naamini nakwenda kumzika akapumzike kwa amani”
  Mama Kanumba

Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake.

Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.
Share on Google Plus

0 comments: