*HUYU NDIYE PROF. MKUMBO NINAYEMFAHAMU*
Wakati natafakari kichwani namna ya kumjadili *katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji na mwanachama mpya wa chama cha mapinduzi* nikaona nimjadili kipindi ambacho moja,nilikua nae chuo kikuu kishiriki *DUCE* tukifanya kazi vitengo tofauti,mimi nikiwa idara ya sayansi kitengo cha kemia,yeye akiwa mkuu wa idara ya siasa (art) .
Pili,nitamjadili kisiasa, kwani wakati mimi nikiwa kiongozi wa chadema wa wilaya,yeye alikuwa mshauri wa masuala ya siasa makao makuu na mwandishi wa hotuba za viongozi.
La kwanza,Pale *DUCE* wanafunzi na wafanyakazi walikuwa na imani nae,kwenye kazi zake.
Pale DUCE kuna idara/facult tatu,katika idara zote *Prof.Mkumbo* ndiye aliyeleta ufanisi mkubwa katika idara yake kwa kuwafanya wafanyakazi walio chini yake kipindi cha likizo ndefu wawe na kazi za kufanya.
Alianzisha kozi fupi ambazo ziliwainua wafanyakazi wa chini kiuchumi na kiweledi,hili walilisema kwa uwazi kabisa kuwa jamaa anafaa kupanda mpaka juu zaidi ya mkuu wa idara.
Kusema ukweli idara nyingine za sayansi na jamii wafanyakazi wake wengi walikuwa wanaombea kupata mkuu wa idara kama *Profesa Mkumbo* kwani likizo ndefu ya miezi minne kwa wanafunzi,idara nyingine walikuwa wapiga soga wakubwa chuoni,ilihali wafanyakazi wa idara ya *Profesa Mkumbo* wakiwajibika kuingizia idara kipato, chuo kipato,taifa kipato na wao kipato.
Nakumbuka niliwahi ingia mtafaruku na idara yangu ya sayansi,hoja yangu ilikuwa ni kukataa porojo za malecturer wanaofundisha sayansi kutoa mafunzo ya vitendo kwa kiwango kibovu.
Nilimuendea *Prof Mkumbo* kumueeleza,akasifia na akaniambia niandike proposal namna bora baadae ya kutoa mafunzo.
Akanielekeza namna ya kuandika,na niliandika kwa kifupi na siku ya kikao cha kunisulubu nikawasilisha karatasi *concept paper* hiyo namna bora ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi,pia niliongeza kwa watu wa nje yaani mafunzo ya *ujasiliamali* wasio wanafunzi.
Na hii niliitengeneza iwe kipindi cha likizo ndefu na fupi na siku za mwisho wa juma.
Karatasi ile aliyonielekeza prof.Mkumbo yaani *concept paper* niliwasilisha na joto viongozi wangu wa juu likapoa.
Japo baadae nilifukuzwa baada ya kutekwa sijui liliendelea vipi.
Hakika *Prof Mkumbo* kwenye suala la maendeleo ya chuo alikuwa yuko tiyari kwa lolote,ilimaadamu alete ufanisi kwa chuo kizima.
Nakumbuka benki kuu ilileta vifaa vya maabara ya Chemia,Siku hiyo alipita akatueleza watu wa maabara,jamani tambueni vifaa hivyo ni ghari sana serikali imenunua,viangalieni sana,akanitania *Yona* angalieni sana.
*Profesa Mkumbo* alikuwa ananiambia chuoni si mahali pa kuleta siasa ni mahala pa kuwatoa wasomi ambao watalisaidia taifa,na hata kama ni wanasiasa,wawe wanasiasa wenye akili wa kuliletea taifa maendeleo na amani. Aliniambia siasa ziwe za kujenga na si kelele tu bila maendeleo.
La pili,akiwa mshauri wa *chadema* aliweza kufanya vitu ambavyo kweli vilionekana kwa macho,kwa mfano aliweza kuandika ilani ya uchuguzi nzuri zaidi,ambayo iliwaibua wasomi na wasio wasomi kumsikiliza *Dr. Slaa* aliyekuwa mgombea urais mwaka 2010.
Kwa kifupi nikiwa kiongozi wa chadema,nilimfahamu *Prof Mkumbo* aliyekuwa mshauri wa chama kwa kuwa muandishi mzuri wa hotuba za viongozi wakuu zenye mvuto.
Alikuwa ni msomi ambaye kabla ya wahafidhina kuvamia chama,aliweza kuendeshaa midahalo, Kushiliki midahalo na kuelezea dira ya chadema mbeleni na hii ilitoa mwelekeo wa baadae.
Aliweza kuwakilisha chama kwenye vipindi vigumu,mfano alifanikisha kuendesha itifaki nzima ya msiba wa *Mzee Bob –Makani* viwanja vya karimjee, mimi nikiwa kwenye kukaribisha viongozi wakuu wa nchi,vyama na serikali yeye alikuwa mtangazaji wa matukio yote na kuruhusu itifaki zote kwenye msiba ule mzito kwa chama.
Pamoja na mambo mengi ndani ya chama ya kushauri,bado *Prof Mkumbo* ni mtu ambaye yeye propaganda za uongo haziwezi,alikuwa ni mtu wa kusema ukweli kama alishiriki jambo alisema tu bila kuogopa,mfano kwenye kikao cha kamati kuu chá chadema,wakati wanaujadili *waraka wa mabadiliko 2013* alisema kwa uwazi alishiriki kuandika,hii ilimbeba sana kwa washirikisha ubongo. Taifa lazima liwe na viongozi wakweli ili tufike.
Leo hii uongo ni fasheni kwa viongozi wetu na wabunge walio wengi,wanaoonekana wako makini kwa uongo wa data za kumhonga mtumishi na mtumishi wa Uma kwa kuwa Ana Shida na pesa anakupikia data za uongo, na wanasiasa uchwara huwasilisha tu.
Ndo maana leo hii Mtu kama *prof Mkumbo* kwenye awamu hii ya Ukweli wanahitajika sana.
Sema nimekuja kugundua kuwa maisha ni maisha tu,kuwa staili inayotumika hata kwenye vyama kuwa waweze fanya mema 1000,lakini baya moja tu hata la kutungwa ukaonekane mbaya,Msaliti nk.
Mema aliyoyafanya *prof.Mkumbo*kila mtu ndani ya *chadema* anajua,leo maneno ya abanuasi ya kufikirika,ya kutungwa yamemuondolea uhalali, aah!!!,Kwenye chama chao kitukufu.
Baada ya maelezo hayo hapo juu pia naomba nijieleze tarehe 4 april 2014 hadi tarehe 5,april 2014 siku ambayo nilihudhulia/nilikalibishwa wakati wa mchakato endelevu wa uanzishaji *ACT-Tanzania* kwa sasa *ACT-wazalendo* katika ukumbi wa Edema(Edema conference center) morogoro msamvu jirani na chuo Kikuu cha Kiislam.
Kikao hicho ambacho yalizungumzwa mengi sana ya kujenga chama kipya chenye uzalendo Tanzania,tulimuomba na kumkalibisha *prof. Mkumbo* ambaye alikua na semina zake maneo hayo,kipindi kidogo viongozi wakaona ni vizuri awepo.
Leo hii ninapotafakari,na ninapoona yale yote ambayo tulikubaliana pale msamvu kwa msingi baadhi ya watu walikiuka makubaliano hayo kwa vipesa vya kuhaidiwa tu.
Wakati naangalia leo *ACT-wazalendo* walipo na wanapoelekea ndipo,napata ujasiri kabisa wa kusema mtu kama *Prof. Mkumbo* anahitajika kulisaidia taifa letu.
Tukiwa kwenye kikao pale msamvu wa muda kwa siku mbili,ndipo *Pro.Mkumbo* alielekeza viongozi namna ya kuwa na chama kisicho na mashaka kwa watanzania wote,wakiwemo wasomi ambao wengi hawajaona chama chenye matumaini kwao mbeleni.
*Prof.Mkumbo* alielekeza chama lazima kiwe na misingi,hapa alielekeza misingi kumi ya kuwa chama mfano *uzalendo,umoja,utu,usawa,uwazi,udilifu,uwajibikaji,demokrasia uhuru wa mawazo na matendo na kupiga vita rushwa*.
Pia alielekeza chama lazima kiwe na nguzo tano ambazo ndio imani ya chama,ambazo imani zilizotuvutia sana ni *kuimarisha mapambano dhidi ya dhuluma,fitina,unafiki,uongo,rushwa na ufisadi*.
*Kupambana na umaskini na kusimamia utajiri wa nchi yetu kwa faida ya wote*.
*Kushiriki kujenga taifa linalojitegemea,lenye msingi ya haki,lisilo na unonyaji na ubaguzi*.
*Pro Mkumbo* Alisema lazima tujenge chama mbadadala ambacho kivutie kila mtu,na akashauri chama kisiwe na mjomba, *Hapa ndipo Act-wazalendo imeharibikia*).
Alishauri lazima kijengwe chama chenye *falsafa,itikadi,malengo na muelekeo ambao watu watakuwa na imani nacho*.
Alionya kwenye chama kusiwe na waasisi wa Chama,wenye Chama ,mwenye chama,lazima ijengwe taasisi ambayo wote ni wanadamu ikitokea la kutokea chama kiwepo .
Yaani kila mtu ndani ya chama ajione ni mwenye chama,na ashiriki chaguzi zozote bila kubaguliwa,au kwa kiini macho,na pia isitokee Mtu akasema bila yeye hakuna chama yaani chama hakiwezi kufa Labda afe yeye kwanza.
Leo hii watanzania tambueni *misingi,nguzo,itikadi,falsafa wanazokimbia nazo ACT-wazalendo nchi nzima ni msingi uliojengwa na prof.Mkumbo* na zimekuwa kivutio sana.
Leo hii ninapoona *ACT-wazalendo kwa kupitia kiongozi mkuu wa chama niliyekuwa na imani nae zamani Zitto Kabwe*akiamua kwa makusudi kupambana na serikali tuliyoipigania zamani,tena kwa makusudi kabisa akiamua kuwabagua watu wa *chato* kama hawafai kupewa maendeleo yoyote ndo maana Nasema ile misingi aliyoijenga *Prof Mkumbo*kwenye chama cha Act wazalendo inakufa.
Mwisho Nasema kwa haki na kutoka kwenye mtima na sakafu ya moyo wangu,Chama Cha Mapinduzi *CCM* kimempata Mtu sahihi kwa wakati sahihi.
Katika sekta ya maji na umwagiliaji ni muhimu sana kuwa na mtu makini na mfuatiliaji kama *Prof Mkumbo* naamini wizarani wanamuona katibu mkuu mwenye kuguswa na Shida za Watanzania.
Hongera sana kiongozi wangu,mtani wangu,rafiki yangu *Prof Kitila Mkumbo*karibu Chama makini CCM.
*Safari ni Safari*
Nawasilisha ni Yona Mkiti wa CCM tawi la Bokorani.
About author: PAVEA BLOG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: