Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon
***
Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya
Acacia, Brad Gordon na ofisa mkuu wa fedha Andrew Wray wamejiuzulu,
kampuni hiyo ya uchimbaji wa madini imetangaza.
Kampuni hiyo yenye migodi mitatu ya
dhahabu kaskazini magharibi mwa Tanzania imetangaza kuwa wawili hao
wataondoka rasmi Acacia mwishoni mwa mwaka huu. Hata hivyo, taarifa
inayopatikana kwenye tovuti ya kampuni imeeleza kuwa, Peter Geleta
ataiongoza kampuni hiyo katika kipindi cha mpito huku Jaco Maritz
akiongoza kitengo cha fedha.
Wateule hao wataanza kazi kuanzia
Januari 1, mwaka kesho. Akizungumzia kujiuzulu kwa Brad na Andrew,
mwenyekiti wa Acacia, Kelvin Dushnisky amenukuliwa na taarifa hiyo
akisema, “Brad na Andrew wamekuwa kiungo muhimu katika uendeshaji na
masuala ya fedha hapa Acacia kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne. Kwa
niaba ya bodi, ninapenda kuwashukuru kwa mchango wao kwenye kampuni.
Tunawatakia kila la heri kwa siku za usoni.”
0 comments: