Mkazi
wa Ipililo wilaya ya Maswa Mkoani Shinyanga, Salum Nkoja (22)
amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Kisutu akikabiliwa na kosa la
mauaji ya kukusudia ya mtu asiyefahamika.
Hata
hivyo, kwa taarifa zilizoko inadaiwa mshtakiwa huyo alikamatwa na
viungo vya binadamu zikiwemo sehemu za siri wanawake. Mshtakiwa
alisomewa kosa lake na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambapo amedai mshtakiwa anakabiliwa
na kosa moja.
Katuga
alidai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la mauaji kwa kukusudia ambalo
amelitenda kati ya October 1 na 30, 2017 katika sehemu isiyofahamika
kati ya Ubungo Dar es Salaam na Kahama.
Wakili Katuga alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Baada
ya kusomewa kosa hilo, Hakimu Mkeha alimtaka mshtakiwa asijibu chochote
kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji,
ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi December 8, 2017.
Katika
taarifa zilizopatikana inadaiwa mshtakiwa huyo alikutwa na sehemu za
siri za binadamu zilizokaushwa ambazo ni za wanawake.
0 comments: