NYOTA
wawili wa kutumainiwa wa klabu ya Simba, Mlinda mlango Aishi Manula
pamoja na kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya, wamepokea viatu vyenye
thamani ya Sh 500, 000 kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.
Wawili
hao walikabidhiwa viatu hivyo aina ya CR7 Mercurial kutoka kampuni ya
Nike, mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya
Lipuli, ulioisha kwa sare ya bao 1-1 uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru,
Dar es Salaam.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa viatu hivyo, Manula alisema anajisikia fahari
kupata zawadi hiyo kutoka kwa mashabiki hao ambao wameonyesha upendo
wao kwake na kuahidi kuendelea kufanya vizuri ili kuwafurahisha zaidi.
“Ni
jambo zuri ambalo linatia hamasa ya kuendelea kujituma zaidi na
kuisaidia timu kufanya vizuri zaidi katika michezo ya ligi kuu ili
tuweze kutimiza malengo yetu,” alisema.
0 comments: