Ofisa TRA aliyekutwa akimiliki mali na kuishi maisha yasiyolingana na kipato chake halali kusomewa maelezo ya awali (PH) Desemba 6, 2017


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, kesi dhidi ya Afisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi anayekabiliwa na mashtaka mawili ikiwamo la kukutwa akimiliki mali  na kuishi maisha yasiyolingana na kipato chake halali atasomewa maelezo ya awali (PH). Desemba 6 mwaka huu

Jennifer ambaye yuko nje kwa dhamana ameshtakiwa chini ya kifungu cha 27, (1) (a) na (b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Keai hiyo ilikuja leo kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa PH lakini Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter alidai bado hawajamaliza kuandaa maelezo hayo kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa

Hakimu Shaidi aliiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 6 mwaka huu.

Katika kesi hiyo mshtakiwa anadaiwa kuwa  kati ya Machi 21, mwaka jana na Juni 30, mwaka huu  jijini Dar es Salaam  akiwa  mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akimili magari 19

Magari hayo ni   Toyota RAV4, Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Viz, Suzuki Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish, Toyota Mark II, Toyota Wish na  Toyota Mark X.

Mengine ni Toyota Regiusage, Toyota Estimated, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown,  Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Passo na Suzuki Carry yote yakiwa na thamani ya Sh 197,601,207 Mali ambayo hailingani na kipato chake halali.

Pia anadaiwa kati ya Machi  21 ,2012 na  Machi 30,2016 Dares Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akiishi maisha ya kifahari  yenye thamani ya Sh 333,255,556.24 fedha ambayo hailingani na Kipato chake halali
Share on Google Plus

0 comments: