Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa *PAUL MAKONDA* leo amepokea zaidi ya *Tani 405 za Nondo* kutoka kiwanda cha *AM Steel and Iron Mills Ltd* na Mifuko ya *Saruji 500* kutoka *Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa LAPF* kwaajili ya Ujenzi wa *Ofisi 402 za Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari* Dar es Salaam.
Nondo hizo zenye thamani ya zaidi ya *Shillingi Million 150* zimetolewa kama utangulizi ambapo Kiwanda hicho kimesema kitatoa *Nondo za kujenga ofisi zote 402 za Walimu.*
Akipokea Nondo hizo *RC MAKONDA* ameshukuru kiwanda hicho kwa kuunga Mkono kampeni hiyo inayolenga *kurejesha heshima kwa walimu* na kuwapa *morali ya kufanya kazi* ili kuleta matokeo chanya kwa Wanafunzi.
Wakati huohuo *Mfuko wa hifadhi ya Jamii LAPF* umemkabidhi *RC MAKONDA* Kiasi cha Shillingi *Million 5* kwaajili ya kununua *Mifuko 500 ya Saruji* za Ujenzi wa Ofisi za Walimu.
*RC MAKONDA* amewahimiza Wananchi na wadau kuendelea kuchangia kampeni ya ujenzi wa Ofis za walimu kupitia *Saruji, Kokoto, Mchanga, Nondo Mbao, Milango, Madirisha na Bati* ili kufanikisha kampeni hiyo.
Kwa upande wake *Mkurugenzi* wa Kiwanda hicho *Shekh SHAHID SALIM* amesema watatoa kiasi chote cha mahitaji ya Nondo zinazohitajika kwakuwa *wanatambua umuhimu wa Walimu na kazi* kubwa anayoifanya *RC MAKONDA* kwenye Mkoa wa Dar es Salaam.
Nae Meneja Masoko na Mawasiliano LAPF *Bwana JAMES MLOWE* amesema kuwa wameamua kumuunga mkono *RC MAKONDA* kwakuwa fedha zinazotolewa kwake zinafanya kazi iliyokusudiwa.
*Tayari kasi ya ujenzi wa Ofisi za walimu inaendelea katika Shule mbalimbali jijini Dar es Salaam.*
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: