Ruge
amezungumzia suala hilo ikiwa ni wiki kadhaa tangu isambae sauti
iliyoaminika kuwa ni ya kwake, akisikika mtu anazungumza na Zamaradi
kwenye simu huku akilia kwa sauti ya mateso akilalama kuachwa.
Amesema
kuwa kama mwanaume muungwana, huwa hazungumzii masuala ya ndani ya
mahusiano yake ya kimapenzi, akitumia msemo wa kiingereza kuwa
‘Gentlemen don’t kiss and tell’, kwa tafrisi isiyo rasmi ‘hatubusi na
kusimilia’. Msemo huu una maana ya kuwa wanandani hawasimulii kuhusu yao
ya ndani.
Ruge
amesema kuwa alikuwa anafahamu kila kilichokuwa kinaendelea kuhusu ndoa
ya Zamaradi na kwamba alikuwa amempa baraka zote tofauti na ilivyokuwa
ikizungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameshtukizwa na kuumizwa.
“Kila
kilichofanyika nilikuwa na taarifa na kilikuwa na baraka zangu. Ni
sehemu ya maisha tunapitia. Kubwa kuliko yote, nina watoto wawili ambao
nimezaa na Zamaradi. Nina mheshimu mno na hadi sasa naendelea kumheshimu
mno,” Ruge amefunguka kupitia kipindi cha Clouds 360.
“Unajua
kama kuna kitu nitakufundisha [mtangazaji] kama mdogo wangu , ‘When you
are a gentleman, you don’t kiss and tell’ (Ukiwa mwanaume muungwana,
haubusi na kusimulia). Vitu vingine vinabaki kuwa vyako binafsi vya
ndani,” aliongeza.
Ruge
ameeleza kuwa hata wikendi iliyopita alikuwa na watoto wake aliozaa na
Zamaradi na kwamba anawapenda sana na hataacha kumheshimu mama yao.
Amesema amelazimika kulizungumzia hilo ili kuweka kumbukumbu sawa na sio vinginevyo.
Zamaradi
alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV. Alikifanya
kipindi hicho kuwa maarufu huku akishiriki kuandaa filamu zilizoshika
mitaa ikiwemo filamu ya ‘Kigodolo’.
0 comments: