Shirika
la habari la Bloomberg limesema watu 201 wakiwemo wafanyabiashara,
mawaziri na wana wa ufalme miongoni mwao mwana mfalme Alwaleed bin Talal
anayemiliki jengo refu la ghorofa katika mji mkuu, Riyadh wanashikiliwa
na mamlaka za Saudi Arabia katika kampeni yake ya kukabiliana na
rushwa. Pia, mamlaka zimefunga akaunti zao za benki.
Taarifa
za vyombo vya habari zinasema kuwa mamlaka nchini Saudi Arabia
zimewataka wanaoshikiliwa kurudisha mali walizopata kwa njia ya rushwa
ikiwa wanataka kuachiwa huru na wasifunguliwe mashitaka. Inakadiria kuwa
kati ya dola za Marekani 50 bilioni na 100 bilioni zitahamishwa kwenda
hazina ya taifa.
Mapambano
dhidi ya mafisadi yanaongozwa na mwana mfalme Mohammed bin Salman
anayejaribu kuimarisha nguvu yake ya kimamlaka kabla ya kuapishwa rasmi
kuwa mrithi wa ufalme.
0 comments: