Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amewaomba Watanzania kukichangia Chama hicho ili kiweze kuwafikia na kuwaeleza mambo makuu mawili wakati wa mikutano ya kampeni ya udiwani.
ACT-
Wazalendo imesimamisha wagombea 28 kati ya 43 katika uchaguzi mdogo wa
udiwani utakaofanyika Novemba 26 ambapo kampeni zake zimeanza Oktoba 29.
“Nachukua
fursa hii kuwaomba Watanzania wenye uchungu na nchi yetu kuchangia
kampeni zetu. Tunataka kufika kila ya kona ya nchi yetu na wewe ndio
utatuwezesha kufika,” amesema Zitto
“Chochote
ulicho nacho tunaomba utuchangie kwa kutumia namba hizi hapa. Tigo pesa
0713957977 na M-Pesa 0744959112, Asante Sana,” ameongeza
Zitto
ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini Chama hicho kitatumia kampeni hizo
kuwaeleza Watanzania mambo makuu mawili ambayo ameyataja kuwa ni
ukiukwaji mkubwa wa haki za wananchi na hali ngumu ya maisha ya
wananchi.
“Lengo
kubwa ni kuwaamsha Watanzania kukataa ubinywaji wa haki za binaadamu na
kutaka mabadiliko ya sera za uchumi ili kuongeza ajira na kuondoa
umasikini,” amesema Zitto
Amesema watatumia mifano halisi kwenye kata husika na kutoa sera mbadala kwa misingi ya Azimio la Tabora.
0 comments: