JIJI
la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 duniani ambayo yamepata tuzo
ya C40 Bloomberg Philantropies 2017 kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo
Haraka.
Katika
tuzo hiyo mwaka huu imepokelewa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es
Salaam Isaya Miwta aliyerejea nchini alfajiri ya Desemba 8 mwaka huu.
Jiji la Dar es Salaam limechangia tuzo hiyo na Jiji la New York nchini Marekani
Mradi
wa Mabasi yaendayo haraka unawahudumia abiria 200,000 kila siku kwa
kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa
magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa
siri ya mafanikio ya tuzo jijini hapa.
Tuzo
ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka katika miradi
inayotekelezwa kwenye maeneo mahususi matano ili kutambua jitihada za
majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90 duniani
inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya
Tabia ya Nchi Duniani.
Imetolewa Desemba 10
Na Christina Mwagala ,
Afisa Habari Ofisi ya Mstahiki Meya wa jiji.
0 comments: