Shirika
la Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa
ununuzi wa Umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na
wanaweza kununua
katika mifumo iliyozoeleka.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na
Mawasiliano(TEHAMA) wa Tanesco, Demetruce Dashina alisema kuwa kulitokea
tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku kutokana na
wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakihamisha mitambo hiyo kutoka
ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine.
“Jana
tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa luku kwenda katika ofisi zetu
mpya hivyo ikawalazimu wateja wetu kupata usumbufu kidogo, lakini
kuanzia saa saba(jana) mfumo huo umekaa sawa na wateja wanaweza kununua
umeme kama walivyokuwa wanafanya hapo awali bila shida yoyote mara baada
ya marekebisho ya kiufundi” alisema Dashina
Alisema
kuwa shirika lilijipanga kuwahudumia wateja wake kama kawaida wakati wa
kuhamisha mitambo hiyo lakini Wananchi wengi wakapata taharuki hivyo
kufanya mfumo wa
ziada kuzidiwa kutokana na watu kununua umeme kuliko Kawaida.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji aliwaomba
radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa
wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka.
Muhaji
alisema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo kuwataka
watanzania kuwa na Imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya
kuwahudumia kama inavyohitajika.
0 comments: