Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma imesema
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis
atafikishwa mahakamani leo.
Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma, Emma Kuhanga jana alisema Sadifa atafikishwa mahakamani leo Jumatatu Desemba 11,2017.
Alisema
kiongozi huyo alikamatwa nyumbani kwake akiwapa soda wajumbe wa UVCCM
kutoka Mkoa wa Kagera kitendo ambacho ni kinyume cha maadili.
UVCCM
jana Jumapili Desemba 10,2017 ilichagua viongozi wapya wa ngazi ya
Taifa watakaoongoza jumuiya hiyo ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano.
Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge, Zanzibar alikamatwa nyumbani kwake Mailimbili mjini Dodoma.
0 comments: