Wakili Mabere Marando aliyekuwa
akimtetea mwanamuziki mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na
mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, amesema uamuzi wa Rais John
Magufuli kuwasamehe umekuwa ni ‘surprise’ (jambo la kushtukiza) kwake.
Babu Seya na Papii Kocha ambaye pia ni
maarufu kama Mtoto wa Mfalme walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha
jela kwa kosa la kuwabaka na kuwalawiti watoto 10 wa kike ambao walikuwa
wanafunzi wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza Dar es Salaam.
Tayari walishatumikia kifungo hicho kwa miaka 13 na miezi minne.
Wakili Marando ambaye aliwatetea katika
rufaa yao ya pili Mahakama ya Rufani alisema uamuzi wa Rais Magufuli
umemshangaza na ameupokea kwa furaha kubwa.
Marando ambaye alifanikiwa kuwatoa
kifungoni watoto wawili wa Babu Seya, Mbangu na Francis katika rufaa
hiyo alisema hakutarajia uamuzi kama huo.
“Asante sana, asante sana, asante sana,
namshukru sana Rais Magufuli kuwasamehe, kwa kweli sikutarajia hili. Hii
imekuwa ni surpirise, asante sana,” alisema Wakili Marando ambaye
alikuwa hajapata taarifa za uamuzi huo hadi alipoulizwa na mwandishi
wetu.
0 comments: