Sunday, December 10, 2017
Naibu
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, ameungana na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika kuomboleza vifo
vya askari 14 waliouawa nchini Kongo na wengine kujeruhiwa, huku akiwapa
pole wafiwa wote.
Mbunge
wa Kibamba ameitumia Jumapili ya leo Disemba 10,2017 kuwaombea
mashujaa hao na kuwapa pole wanafamilia wote ambao ndugu zao wamepoteza
maisha katika tukio hilo.
"Kwa
kipekee naitoa ibada ya leo kuwaombea Mashujaa wetu,askari 14 wa JWTZ
waliojitoa mhanga na maisha yao kuitetea amani Congo, 44 ambao
wamejeruhiwa na wale wawili (2) ambao hawajulikani walipo. Mungu
awajalie pumziko jema kwa wale waliopoteza uhai kupigania amani
"Awape
uponyaji majeruhi na kusaidia kupatikana kwa Askari wawili. Aijalie
faraja na ustawi familia za wahanga na wote ambao wameguswa kwa moja kwa
moja au namna ingine yeyote na tukio baya hilo" aliandika John Mnyika
0 comments: