Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli amewataka wajumbe wa Baraza Kuu wa Umoja wa Wanawake CCM(UWT) kuchagua viongozi ambaye atakuwa anajali wanawake na siyo kujali tumbo lake.
Akizungumza na wajumbe hao leo Ijumaa wakati akifungua mkutano huo Rais Magufuli amesema watakapokuwa wanachagua viongozi leo Ijumaa wasiangalie wamepewa kanga kiasi gani, wala amelipiwa hoteli ya aina gani.
“Nataka mchague kiongozi wa kujali wanawake na sio kujali tumbo lake na awe mtetezi na shida zao wala habagui,” amesema Rais Magufuli.
Amesema anawapenda akina mama hivyo wachague mtu kwa matakwa yao.
“Viongozi wa jumuiya hii wanatakiwa kujua historia na kuipigania jumuiya hii muhimu kwa CCM,”
“Wanawake ndio wapigaji kura waaminifu na ukiahidiwa kura nao jua utashinda.”
Amesema, “Chama tunakata kiwe cha wananchi na sio cha mtu binafsi na kiongozi atakayechaguliwa aendane na mabadiliko ya ndani ya chama.”
0 comments: