Rais Magufuli: Wanaosema Vyuma Vimekaza Waweke Grisi la Sivyo Vitavunjika

 

Rais John Magufuli amesema vyuma vikikaza vinatakiwa kuwekwa grisi vilainike, vinginevyo vitavunjika kabisa.

Amesema hayo leo Alhamisi Desemba 14,2017 alipofungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Rais Magufuli amesema waliokuwa wanapata fedha kwa njia zisizo halali ndiyo wanaosema vyuma vimekaza.

“Vyuma vimekaza na bado vitavunjika kabisa nawashauri muweke grisi,” amesema.

Msemo wa vyuma vimekaza umekuwa maarufu katika siku za karibuni ukiwa na maana maisha yamekuwa magumu.

Rais Magufuli amesema alipoingia madarakani alikuta changamoto nyingi zikiwemo za wafanyakazi hewa, vyeti feki na ufisadi. 

Amesema baada ya kudhibiti, watumishi wa umma 12,000 wamepatikana na vyeti feki wakiwemo walimu 3,655 tangu walipoanza kuhakiki.

Amesema uhakiki huo ulibaini watumishi hewa 20,000 na kwamba, Serikali ilikuwa inapoteza fedha nyingi kuwalipa mishahara.

“Kila kitu kilikuwa hewa hata mapenzi inawezekana yalikuwa hewa,” amesema Rais Magufuli.

Amesema kutokana na udhibiti wa fedha za Serikali ni lazima watu waliokuwa wanapata fedha kwa njia zisizo halali watalalamika kuwa vyuma vimekaza.

Kuhusu madai ya walimu, amesema Sh25 bilioni wanazoidai Serikali zitalipwa baada ya uhakiki kumalizika

==>Msikilize hapo chini

Share on Google Plus

0 comments: