Njama 638 za mauaji alizoepuka Fidel Castro

Fidel Castro akivuta sigara yake 

Fidel Castro akivuta sigara yake

Njama ya kutumia sigara kumuua Fidel Castro ambayo ilitibuka inajulikana sana, lakini njama nyengine 637 dhidi ya maisha yake ni zipi?
Shirika la kijasusi nchini Marekani CIA na watu waliotoroka Cuba wakati wa uongozi wa Castro walitumia nusu ya karne moja kufanya njama za kumuua kiongozi ambaye taifa lake lina athari kubwa kwa Marekani, kulingana na balozi wa Marekani nchini Cuba Wayne Smith.

Wakati mmoja kiongozi huyo wa Cuba alinukuliwa akisema, iwapo kuepuka majaribio ya mauaji kungekuwa miongoni mwa michezo ya Olimpiki ningejishindia medali ya dhahabu.
Hatahivyo baadhi ya njama hizo hazikutekelezwa ,kulingana na aliyekuwa mlinzi wa zamani wa Fidel Castro, Fabian Escalante.




Mpenzi wa zamani wa Castro, Marita Lorenz alipewa dawa za sumu kumwekea katika kinywaji chake
 Mpenzi wa zamani wa Castro, Marita Lorenz alipewa dawa za sumu kumwekea katika kinywaji chake.

Stakhabadhi zilizofichuliwa wakati wa utawala wa Bill Clinton zilionyesha kuwa CIA wakati mmoja walianza kuwafanyia utafiti konokono wa eneo la Carebean.
Njama, ilikuwa kutafuta konokono mmoja ambaye angemvutia Castro anayependa sana kuogelea na kumjaza vilipuzi ndani yake kabla ya kumlipua Castro atakapomshika
Mpango mwengine ulikuwa ule wa kutengeza boya la kuogelea ambalo huvaliwa kama shati na ambalo lingetiwa ugonjwa mbaya wa ngozi ili kumuathiri kiongozi huyo.
Mipango yote hiyo ilitupiliwa mbali.
Ajenti huyo alisikitika na akataka mpango mwengine ambao sio rahisi kuugundua,ripoti hiyo ilisema.


Mmoja ya wapenzi wa Castro wa zamani ,Marita Lorenz alisajiliwa.
Alipewa dawa zenye sumu ili kuweka katika kinywaji cha Castro.Lakini Castro aligundua jaribio hilo na anadaiwa kumpatia bunduki yake badala yake atumie kumuua.
''Huwezi kuniua. Hakuna anayeweza kuniua,"Bbi Lorenzo alisema Bw Castro alimwambia, alipokuwa anahojiwa na gazeti la New York daily.

Castro alidaiwa kutabasamu na kuendelea kuvuta sigara yake.''Nilijihisi nimetolewa pumzi kwa sababu alikuwa na uhakika juu yangu.Alinikumbatia na tukafanya mapenzi''.

Jaribio jingine lililokuwa maarufu dhidi ya maisha ya Castro ni lile la 2000, wakati ambapo mpango uliwekwa kuweka vilipuzi vingi katika jukwaa ambalo alitarajiwa kuhutubia nchini Panama.

Mpango huo ulitibuliwa na vikosi vya usalama vya Castro.
Watu wanne ikiwemo mtoro mmoja wa Cuba pamoja na ajenti wa CIA kwa jina Luis Posada walifungwa lakini baadaye wakaachiliwa.
Pia kulikuwa na mipango ya kumfanya Castro ambaye pia anajulikana '' The Beared'' aonekana kama chombo cha kukejeliwa badala ya kumuua.
Mpango mmoja ulikuwa kumwagia viatu vyake chumvi ya thallium wakati wa ziara yake ya ughaibuni kwa lengo kwamba anaposhika ndevu zake zingeweza kukatika.
Lakini mpango huo ulitibuliwa baada ya Castro kuahirisha ziara hiyo.Castro alichukua tahadhari ya hali ya juu ili kuwakwepa watu waliopanga mauaji yake.
Mwaka 1979 alipokuwa akielekea mjini New York ili kuhutubia mkutano wa Umoja wa Mataifa hakuweza kuwazuia wanahabari waliomuuliza iwapo alikuwa amevaa fulana ya ndani ambayo ina kinga dhidi ya risasi, alivua shati lake na kuwaonyesha kifua chake.

Mtanzania afungua mgahawa Sweden

TanzaniaIssa Kapande `Chef Issa.

Mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa', umefunguliwa nchini Sweden na kuvunja rekodi ya dunia.
Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.

Balozi Msechu alimpongeza Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya.

Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.
Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi alielezea kufurahishwa na juhudi za Kapande.

Alisema Issa ameonesha njia kwamba inawezekana kwa watu waliopo Ughaibuni sio tu kuajiriwa, bali kujiajiri katika nyanja mbalimbali.Alisema hilo linawezekana kutokana na kufuatilia kwa karibu taratibu za wenyeji na kisha kutumia mafunzo yaliyopo kukamilisha ndoto.

"Ni dhahiri kuwa, Chef Issa kwa kupitia taaluma yake ya upishi amewezeshwa kumiliki mgahawa huu hapa Trollhattan,S weden kwa hilo, napenda tuishangilie na kuipigia makofi Sweden na Trollhattan."Alisema akimpongeza kijana huyo ambaye pia amewekeza mkoani Mtwara.

Katika mahojiano, Mpishi Mkuu Issa Kapande alisema mafanikio yake yanatokana na juhudi kubwa na nia aliyoiweka katika kujifunza na kufundisha wengine katika mitandao ya wapishi wakuu.
Alisema akiwa amefanyakazi katika nchi 17 na tayari akiwa na vitega uchumi nchini alianzia nia ya kuwekeza Sweden mwaka 2009 wakati alipohamia nchini humo akitokea Uswisi. Alisema alianza kwa kuomba vibali, lakini mchakato kamili ulianza mwaka 2013."Tulilazimika kufanya utafiti kidogo" alisema na kuongeza kuwa katika utafiti huo walihoji watu 300 na kujua mwelekeo hasa wa shughuli yao unastahili kuwaje.

Kapande ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Manchester Metropolitan na Chuo kikuu cha kimataifa cha menejimenti ya hoteli cha Uswis amesema amepambana vikali na mkewe hadi kufikia hatua ya kuanzisha mgahawa huo ambao upo katika eneo la ukubwa wa skwea mita 810.Kapande ambaye mwaka jana alitwaa tuzo ya dhahabu katika upishi akiwa na timu ya Sweden magharibi alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wapishi wa nyumbani kukubali kubadilika na kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kujifunza na kufunza ili kuwa na aina nyingine ya mapishi katika kuendeleza sekta.

Ndani ya mgahawa huo pia watu mbalimbali watapatiwa taarifa za utalii Tanzania.
Katika kazi yake ya upishi, amebahatika kuwapikia watu mashuhuri duniani, baadhi wakiwa Andrew Young, Mchungaji Jesse Jackson, Robert Mugabe (Rais wa Zimbabwe), Paul Kagame (Rais wa Rwanda), Benjamini Mkapa (Rais mstaafu wa Tanzania), Raila Odinga (Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya), Daniel Arap Moi (Rais Mstaafu wa Kenya), Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton na mumewe Bill Clinton, Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Laura Bush.

Wengine ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, mwigizaji Chris Tucker, Rais wa zamani wa Afrika Kusini hayati Mzee Nelson Mandela, Koffie Olomide, Youssour ndour, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal ya England), Gianluca Vialli (nyota wa zamani wa Italia aliyewahi kuichezea na kuinoa Chelsea ya England), Rais wa Congo DRC, Joseph Kabila, Billy Gates na wengine wengi.

White House: Madai Dhidi ya Trump hayana msingi

Ikulu ya White House imesema hakuna ushahidi wowote wa kuashiria kwamba kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi mkuu wa Marekani uliofanyika tarehe 8 Novemba.
 Bw Josh Earnest alisema madai ya Bw Trump hayana msingi
Afisa wa habari wa ikulu Josh Earnest amepuuzilia mbali madai ya rais huyo mteule kwamba mamilioni ya watu ambao hawakufaa kupiga kura walishiriki katika uchaguzi huo.
Bw Trump alikuwa pia amedai kwamba kulitokea wizi wa kura katika majimbo ya Virginia, New Hampshire na California, majimbo ambayo Hillary Clinton alishinda.

"Ninachosema ni ukweli mtupu, kwamba hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai kama hayo," Bw Earnest aliambia wanahabari White House.
Bw Trump, aliyeshinda uchaguzi kwa kupata kura nyingi za wajumbe, alikuwa amelalamika kuhusu uchaguzi huo kupitia Twitter Jumapili.

"Licha ya kushinda Kura za Wajumbe pakubwa, pia nilishinda kura za kawaida ukiondoa kura za watu ambao hawakufaa kupiga kura lakini walipiga."
Kwenye ujumbe wa kufuatiliza, aliandika: "Ingekuwa rahisi zaidi kwangu kushinda kura za kawaida kuliko Kura za Wajumbe kwa sababu ningehitajika kufanya kampeni katika majimbo 3 au 4 badala ya majimbo 15 ambayo nilitembelea.
"Ningeshinda kwa urahisi hata zaidi na kwa njia ya kuridhisha (lakini majimbo madogo yanasahaulika)!"

Rais huyo mteule alianza kulalamika baada ya maafisa wa kampeni wa Clinton kusema wataunga mkono mchakato wa kuhesabiwa upya kwa kura katika jimbo la Wisconsin ambao ulianzishwa na mgombea wa chama cha Green Party Jill Stein.
Bi Stein pia ameifahamisha bodi ya uchaguzi katika jimbo la Michigan, ambapo ushindi wa Bw Trump wa kura 16 za wajumbe ulithibitishwa Jumatatu, kwamba ataomba kura za urais zihesabiwe upya.
Anapanga kufanya jambo sawa jimbo la Pennsylvania.
Bw Trump alishinda kwa kura chache zaidi jimbo la Michigan katika kipindi cha miaka 75 na ndiye mgombea wa kwanza wa Republican kushinda katika jimbo hilo tangu 1988.
Juhudi za Bi Stein za kupigania kuhesabiwa upya kwa kura zinasaidiwa na kampeni ya mitandao ya kijamii ya #recount2016 ambao imesaidia kuchangishwa kwa jumla ya $6.3m (£5m).
Wakati wa kampeni, alifanikiwa tu kuchangisha, $3.5m.Dkt Jill Stein alikuwa mgombea wa chama cha Green
Ili kubadili matokeo ya uchaguzi, itahitaji matokeo yabatilishwe katika majimbo ya Wisconsin, Michigan na Pennsylvania, jambo ambalo wachanganuzi wanasema ni ngumu mno.
Maafisa wa kampeni wa Bi Clinton walisema watashiriki shughuli ya kuhesabu upya kura jimbo la Wisconsin.
Mshauri mkuu wa kampeni Marc Elias alisema hakuna ushahidi kwamba uchaguzi huo uliingiliwa, lakini "tuna wajibu kwa Wamarekani 64 milioni waliompigia kura Hillary Clinton kushiriki katika shughuli hii inayoendelea kuhakikisha matokeo yanayripotiwa ni sahihi."
Jill Stein, 66, ni daktari na mwanaharakati ambaye alitarajia kupata uungwaji mkono kutoka kwa wafuasi wa Democratic waliomuunga mkono Bernie Sanders ambao walikuwa bado wanampinga Bi Clinton uchaguzini.

VIJANA TEMEKE WAFURAHIA MASHINDANO YA MTONI CUP YA YONA

 Mdhamini wa mashindano ya Mtoni CUP bwana Joseph Yona akiwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa sabasaba Ibrahim Mwita wakati wa Fainali ya Mashindano hayo.

mashindano ya mpira wa miguu ya Mtoni CUP yaliyokuwa yakiendelea katika uwanja wa michezo wa SIFA uliopo mtoni mtaa wa sabasaba yaliyohitimishwa wiki iliyopita, yameibua furaha kubwa kwa vijana wa wilaya ya temeke na kumtaka aliyekuwa mdhamini wa mashindano hayo kuangalia uwezekano wa kuyapanua kufikia ngazi ya wilaya au tarafa ili vijana wengi zaidi waweze kushiriki na kuibua vipaji vingi zaidi.

''ebwana tunamshukuru sana huyu kiongozi, ametuunganisha na ametusaidia angalau kujiburudisha na kuongeza hali ya ushirikiano na wenzetu hapa mtoni. tunamshukuru sana na mungu amuongezee'. alisema Saidi Kimalija wa Mtoni

RAIS MAGUFULI AZIDI KUUNGWA MKONO KILA KONA.

Kada mtiifu na mwanachama kindakindaki wa chama cha Mapinduzi, Joseph Yonah Patrick amesema taifa lina kila sababu ya kujivunia Rais John Pombe Magufuli kutokana na uchapakazi wake na namna alivyojidhatiti kuwaletea mabadiliko ya kweli watanzania chini ya chama cha mapinduzi ccm.
Joseph Yona.
akiongea na mtandao huu Bwana Yonah amesema kuwa kwa sasa hana mashaka na uadilifu na mapenzi ya dhati aliyonayo Rais kwa nchi yake.
''unajua watanzania walijisahau sana, wakawa wanaishi kwa mazoea, nchi ilikuwa inaliwa balaa, hebu fikiria ilikuwa mpaka vijana wanakataa kuajiriliwa na wanaendendelea kupata pesa mitaani, sasa hivi hakuna. Rais kasema asiyefanya kazi na asile''. amesema Yonah.

''mimi nilishiriki kikamilifu kuhakikisha Rais anashinda, nilijitoa kufanya kampeni jimbo la Moshi Mjini, japo Ubunge tulishindwa lakini tunafurahi Rais ameshinda na sasa watanzania hata wa moshi wanaiona faida ya kumchagua JPM. Hongera sana Rais wangu na Mwenyekiti wa chama changu''.
Joseph Yona.

WAFANYABIASHARA WAFURAHIA UTUNZAJI KUMBUKUMBU WA STRAIGHTBOOK

Bi. Maua Rubibi.
umoja wa wafanya biashara ndogo ndogo mikoa ya kigoma,tabora, mwanza na Dar es salaam wamefurahia elimu ya mfumo mpya ya utunzaji wa kumbukumbu za kibiashara zao unaohusisha mauzo na bakaa (stocks) waliyopewa kwa njia ya mtandao wa Whatsapp na Afisa masoko wa taasisi ya Straightbook bi. Maua Ramadhani Rubibi hivi karibuni.

bi maua ameelimisha kuwa Straight ni huduma nafuu yenye  bei tofauti tofauti kulingana na uwezo na uhitaji wa mtumiaji,

 ''Ukitumia online utalipia 20elfu Kwa mwezi, utajiregister Kwenye website yetu www.straightbook.com ila ukifanyiwa installation kuna malipo ya aina tatu, Moja utalipia 25elfu kwa mwezi for single user ila njia ya pili kwa yule hataki kulipia mwezi mwezi atalipia laki5 kisha atatumia mfumo na kulipia laki moja moja kwa ajili ya upgrades na supports kila mwaka Njia ya mwisho ni kununua package na kutumia bila malipo mengine, hii utalipa mill 1.9 (million moja na laki9) utapata free supports na upgrades Kwa kipndi chote na Kwa idadi yeyote ya watumiaji, straightbook haina limit ya users na pia mnaweza kushare kwnye local network moja, karibu sana''.
alisisitiza Bi maua Rubibi

Moto Israel: Washukiwa 12 wakamatwa

Maafisa wa polisi nchini Israel wamewakamata watu 12 kwa tuhuma za uchomaji wa makusudi kufuatia msururu wa moto ambao umekuwa ukilichoma taifa hilo kwa siku nne sasa.
Zima moto wameudhibiti moto huo katika mji wa kaskazini wa Haifa ambapo takriban watu 80,000 walilazimishwa kuondoka.Waziri mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuWaziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Lakini maafisa wanasema moto midogo midogo bado inaendelea kukabiliwa katika maeneo tofauti.
Netanyahu: Moto mkubwa Israel umesababishwa makusudi
Moto huo umesababishwa na hali ya kiangazi pamoja na upepo mkali.
Watu kadhaa wametibiwa kwa kuvuta moshi lakini hakuna majeraha yalioripotiwa.


Waziri mkuu wa Israel awali alisema kuwa iwapo moto huo ulianzishwa kwa makusudi basi washukiwa watakabiliwa na mashtaka ya ugaidi
Kwa Picha: Moto mkubwa watishia Israel
Waziri wa elimu Naftali Bennet ,kiongozi wa chama cha Jewish Home Party ,aliashiria kwamba huenda kuna mkono wa Waarabu ama Wapalestina kupitia ujumbe wake wa Twitter uliosoma: Ni wale wasiotoka katika taifa hili ambao wanaweza kulichoma pekee.
Vuguvugu la rais wa Palestina Mahmoud Abbas, Fatah limesema kuwa maafisa wa Israel wanatumia moto huo kuwalaumu Wapalestina.