BREAKING NEWS: WAHAMIAJI HARAMU WAJIFICHA KWENYE BRIEFCASE

Maafisa wa polisi wa Cueta walichapisha picha hii siku ya JumapiliPICHANI HAWAMIAJI HARAMU WAKIWA KATIKA BRIEFCASE KAMA NGUO.

Maafisa wa polisi wamewakamata raia wawili wa Morocco ambao walijaribu kuwaingiza wahamiaji katika eneo linalotawaliwa na Uhispania lililo kazkazini mwa Afrika la Cueta- wawili hao wakiwa wamejificha ndani ya gari na mwengine katika sanduku waliojaribu kuingia nchini Hispania.
Wakati maafisa wa polisi walipokagua gari moja siku ya Jumatatu ,mtu mmoja alipatikana amefichwa katika eneo la mbele la gari na mwengine amefichwa katika eneo la kiti cha nyuma cha gari.
Mwanamume huyo na mwanamke ,wanaodaiwa kuwa raia wa Guinea ,walipata huduma ya kwanza kwa kuwa walikuwa na hewa kidogo ya kupumua.Mtu mwengine alipatikana amefichwa katika eneo la gari la mbele maarufu dashboardMtu mwengine alipatikana amefichwa katika eneo la gari la mbele maarufu dashboard

Kwengineko kijana mmoja wa asili ya Kiafrika alipatikana amefichwa katika sanduku la mwanamke.
Kisa hicho kilitokea mnamo mwezi Disemba 30 na mtu huyo anayeaminika kutoka Gabon alihitaji matibabu ya dharura.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 22 kutoka Morocco alijaribu kumuingiza Cueta, lakini maafisa wa uhamiaji walimuagiza kufungua sanduku lake ambalo lilikuwa limefungwa katika kitoroli.
Kisa hicho kinajari wakati ambapo kumekuwa na jaribio la wahamiaji wengi kuvunja ua wa mita sita unaogawanya Cueta na Morocco.Mwengine alipatikana amefichwa chini ya kiti hiki kilichotengezwa ili kumtoshaMwengine alipatikana amefichwa chini ya kiti hiki kilichotengezwa ili kumtosha
Raia 50 wa Morocco na 5 wa Uhispania walijeruhiwa wakati wahamiaji 1,100 walipojaribu kupita ua huo na kuingia Cueta kutoka Morocco.
Hakuna aliyefanikiwa kupita ,lakini watu wawili walijeruhiwa walipokuwa wakivunja ua huo na kupelekwa hospitalini huko Ceuta.
Mlinzi mmoja alipoteza jicho lake kulingana na maafisa.
Kisa kama hicho mnamo tarehe 9 Disemba kilihusisha zaidi ya wahamiaji 400 kutoka Afrika.

Wenger: Bao la Giroud miongoni mwa 5 bora

Bao la Giroud dhidi ya Crystal PalaceBao la Giroud dhidi ya Crystal Palace.

Bao la Olivier Giroud la 'scorpion ama nge' katika ushindi wa Arsenal wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace ni miongoni mwa mabao matano muhimu katika uongozi wa Arsene Wenger.
Mabao ya Thiery Henry na Dennis Bergkamp ni miongoni mwa mbao aliyofurahia lakini akasema hili litakuwa 'bao la Giroud'.

Aliongezea: Si bao la kawaida lakini Giroud's alitoa kitu maalum.
Giroud amesema kuwa bao hilo alilifunga kwa bahati.
Uvamizi wa Arsenal katika ngome ya Crystal Palace ulimfanya Giroud kufunga bao hilo maridadi kutoka kwa krosi iliopigwa na Alexi Sanchez.

Guardiola: nakaribia kustaafu kufundisha soka

Guardiola amezifundisha klabu za Barcelona na Bayern Munich kwa mafanikio makubwaGuardiola amezifundisha klabu za Barcelona na Bayern Munich kwa mafanikio makubwa.


Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anakaribia kustaafu kufundisha soka na hataitakuwa miaka 65 kama alivyodhani awali.

Muispania huyo amewahi kuifundisha klabu ya Barcelona ka mafanikio makubwa kisha Bayern Munich kabla ya kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini Man city.
''Nitakuwa hapa Manchester kwa misimu ama mitatu labda na zaidi,'' Guardiola mwenye miaka 45 alisema kabla ya ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Burnley.

''Sitakaa kwenye benchi mpaka miaka 60-65.Nafikiri mchakato wa kuanza kusema kwaheri umekaribia.
Guardiola ameshinda vikombe 14 katika miaka minne akiwa na Barcelona, ikiwa ni pamoja na vikombe vitatu vya La Liga na viwili vya ligi ya mabingwa Ulaya.
Alipumzika mwaka mzima kabla ya kujiunga na Bayern Munich na kuwaongoza kupata vikombe vitatu vya ligi kuu licha ya kukosa ligi ya mabingwa Ulaya
Kikosi cha Guardiola kilicheza pungufu baada ya Fernandinho kupewa kadi nyekundu lakini magoli ya Gael Clichy na Sergio Aguero yaliwapa ushindi.

Trump apuuzilia mbali mpango wa Korea Kaskazini

Donald Trump asema kwamba Korea Kaskazini haitafanikiwa katika mpango wake wa kuunda kombora la masafa marefy litakalofika MarekaniDonald Trump asema kwamba Korea Kaskazini haitafanikiwa katika mpango wake wa kuunda kombora la masafa marefy litakalofika Marekani.

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amepuuzilia mbali madai ya Korea Kaskazini kuwa imeunda Kombora linaloweza kuwasilisha zana za nuklia hadi Marekani.

Katika mawasiliano kupitia mtandao wa Twitter, Bwana Trump aligusia majigambo ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, katika ujumbe wake wa mwaka mpya ambapo alisema kuwa maandalizi ya kombora la aina hiyo yamefikia hatua ya mwisho.

Bwana Trump alisema katika ujumbe wake kuwa "Haitawezekana." Tamko lake la haiwezekani, halikueleweka vizuri kwa sababu wachanganuzi hawajui iwapo alimaanisha kuwa Korea Kaskazini haina uwezo huo au alikuwa akiandaa hatua ya kujikinga.
 Ujumbe wa Twitter wa bwana TrumpUjumbe wa Twitter wa bwana Trump.
 Bwana Trump pia alishutumu Uchina kwa kushindwa kuthibiti mshirika wake Korea Kaskazini na pia akalaumu Beijing kwa kupokea pesa kiasi kikubwa cha pesa na mali kutoka Marekani
BBC

BREAKING NEWS: FANYENI KAMPENI ZA KISTAARABU NA KUFUATA SHERIA ZA NCHI - JAJI MUTUNGI

. http://swahilitimes.com/wp-content/uploads/2016/08/Jaji-Francis-Mutungi.jpgJaji Fransis Mutungi Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini.
Msajili wa vyama vya siasa jaji Fransis MUTUNGI amevitaka vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki chaguzi ndogo za marudio zinazoendelea sehemu mbalimbali  hapa nchini kufanya kampeni za kistaarabu huku wakijikita kwenye kunadi Sera zao na kuwasisitiza waendelee kuliunganisha taifa na sio kushambuliana baina ya vyama wala vyama na serikali.
Jaji Mutungi ameyasema hayo Leo wakati akitoa salamu maalum za mwaka mpya kwa vyama vya siasa na watanzania wote.
"Unajua siasa na wana siasa lazima wakomae sasa,  siasa za kizamani zilikuwa hazinogi kama hakuna kurushiana vijembe, kejeri na Matusi.  Sasa hivi mambo hayo yameshapitwa na wakati na wanasiasa hasa wanaowanadi wagombea wao wahakikishe wanatumia Muda mwingi Zaidi kunadi sera zao kuliko kushambuliana". Alisema Mutungi  
''...unajua siasa.......siasa za chuki zinazogubikwa nakurushiana vijembe....zimeptwa na wakati....''liongeza Jaji Mutungi 
 
JAMVI LA HABARI lilipotaka kujua ni nini ofisi yake inawaahidi watanzania na wafuatiliaji wa siasa kwa mwaka huu mpya 2017 tuliouanza juzi, Jaji Mutungi ameahidi kuendelea kutoa huduma Sawa kwa vyama vyote vya siasa hapa nchini kwa kuwa ofisi yake ina wajibu wa kuvilea vyama hivyo na Demokrasia. ...

kadharika jaji mutungi ameahidi kuendelea kudumisha ukuaji wa demokrasia nje na ndani ya vyama na kuvikumbusha  vyama kujiendesha kama taasisi na kuhimiza vyama kufuata katiba zao na si matakwa ya Viongozi pasipo kuzingatia matakwa ya katiba zao.

nakala ya Calender ya mtandaoni iliyotolewa na msajili wa vyama vya siasa

MBUNGE WILFRED LWAKATARE WA CHADEMA AZIDI KUMWAGIA SIFA RAIS MAGUFULI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbZFNFRxbgCmo0AXDM7jl92VBKcsullj1l2fUbWNN_aSlSGlkCVZYjUzKQLnDrvDaRS9a17kQTHSBD-UANYIKlFQXFZ2bpuZGamrF0Lpi8BFsdgtnd90TymzovUFGGZvhTyTIKfMCNDOg/s1600/IMGS8762.JPGPicha ya Maktaba inamuonyesha Mbunge wa Bukoba Mjini Wilfred Rwakatare CHADEMA akiwa katika viwanja vya bunge akiteta jambo na waziri mkuu Kassim Majaliwa.

katika ukurasa wake wa Facebook ameandika hivi:. 
 
Mimi sina tatizo na Mh Rais Magufuli, anaendesha nchi vizuri.Kilio cha siku nyingi chetu sisi wapinzani ni kumpata Rais anayepinga rushwa na ufisadi kimesikika. Magufuli anaifanya kazi hiyo vizuri .Tumuungeni mkono. Mapungufu yaliyopo yasitufanye vipofu kuona mazuri yake.

Huwa sijibizani na ujinga mitandaoni na hasa kulishwa maneno. Nina uzoefu wa kesi ya kwanza ya ugaidi nchi hii na kilichofanyika kupitia mitandao. Wanaoweka maneno mitandaoni  wanashindwa nini kuweka clip ya video ikionyesha hotuba yangu ya dk 5 niliyoyaongea kwenye Mkutano Bukoba?
Mimi ni nyani mzee,nimeshakwepa mishale mingi. Huo haunipati n'go
3.1.2017.
WILFRED LWAKATARE MBUNGE WA BUKOBA MJINI (CHADEMA)

UMEME VIJIJINI WAING'ARISHA SHINYANGA

VIJIJI 126 VYAPATIA MRADI WA UMEME MKOANI SHINYANGA

ume
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Singida.

WANAKIJIJI wa vijiji 126 wanaopitiwa na mradi mkubwa wa umeme, Backbone wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, wataunganishiwa umeme kwa kulipia kiasi kidogo cha fedha shilingi elfu 27,000/-, tu, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi.Leila Muhaji, (pichani juu) amesema.

Bi Leila ameyasema hayo kwenye kijiji cha Igurubya, mkoani Shinyanga, wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari kutembelea mradi huo, Desemba 22, 2016.
“Nia ya Serikali, kupitia Shirika lake la Umeme nchini TANESCO, ni kuwapatia wananchi wote huduma ya umeme, ambayo ni muhimu katika kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kwa kawaida gharama ya kuunganishiwa umeme kwa vijijini ni shilingi 177,000/- pamoja na kodi ya ongezeko la thamani VAT.” Alisema.

Alisema, kwa kuzingatia hilo, kumekuwepo na juhudi mbalimbali za Shirika la Umeme, TANESCO, kufikisha huduma ya umeme vijijini chini ya mradi wa Wakala wa Usamabzaji Umeme Vijijini (REA), lakini kukamilika kwa mradi huu wa Backbone kutaongeza kasi ya kuwapatia wananchi huduma hii muhimu ya umeme na kwa bei nafuu.” Aliongeza.

 Alisema, Serikali kupitia TANESCO imepiga hatua kubwa ya kuwafikishia umeme wananchi ambapo tayari karibu asilimia 45 ya wananchi wa Tanzania wamepatiwa huduma ya umeme.
Akizungumzia kukamilika kwa mradi huo wa Backbone uliojikita katika kujenga minara na njia za kusafirisha umeme pamona na upanuzi wa vituo vine vya kupoza na kusambaza umeme, Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme, Mhandisi Oscar Kanyama, alisema, mradi huo wa Backbone wa kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400, na urefu wa Kilomita 670, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, umekamilika rasmi Desemba 22, 2016 kwa kuwasha kipande kilichokuwa hakijakamilika cha kutoka Dodoma kwenda Singida.

Mradi huo ulianza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2013 na unafadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo umegharimu karibu shilingi Trilioni 1.
Kazi iliyokuwa ikifanywa ni pamoja na ujenzi wa minara mikubwa yenye uwezo wa kubeba nyaya 6, tatu kila upande tofauti na ile ya awali iliyokuwa na uwezo wa kubeba nyaya 2 tu moja kila upande. “Lakini pia kazi nyingine iliyokuwa ikifanyika chini ya mradi huu, ni upanuzi wa vituo vinne vya kupoza na kusambaza umeme, vituo hivyo ni kile cha Iringa, Zuzu, mkoani Dodoma, Kibaoni mkoani Singida, na Ibadakuli mkoani Shinyanga Shinyanga.” Alifafanua