katika ukurasa wake wa Facebook ameandika hivi:.
Mimi sina tatizo na Mh Rais Magufuli, anaendesha nchi
vizuri.Kilio cha siku nyingi chetu sisi wapinzani ni kumpata Rais
anayepinga rushwa na ufisadi kimesikika. Magufuli anaifanya kazi hiyo
vizuri .Tumuungeni mkono. Mapungufu yaliyopo yasitufanye vipofu kuona
mazuri yake.
Huwa sijibizani na ujinga mitandaoni na hasa kulishwa
maneno. Nina uzoefu wa kesi ya kwanza ya ugaidi nchi hii na
kilichofanyika kupitia mitandao. Wanaoweka maneno mitandaoni
wanashindwa nini kuweka clip ya video ikionyesha hotuba yangu ya dk 5
niliyoyaongea kwenye Mkutano Bukoba?
Mimi ni nyani mzee,nimeshakwepa mishale mingi. Huo haunipati n'go
3.1.2017.Mimi ni nyani mzee,nimeshakwepa mishale mingi. Huo haunipati n'go
WILFRED LWAKATARE MBUNGE WA BUKOBA MJINI (CHADEMA)
0 comments: