. Jaji Fransis Mutungi Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini.
Msajili wa vyama vya siasa jaji Fransis MUTUNGI amevitaka
vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki chaguzi ndogo za marudio
zinazoendelea sehemu mbalimbali hapa nchini kufanya kampeni za
kistaarabu huku wakijikita kwenye kunadi Sera zao na kuwasisitiza
waendelee kuliunganisha taifa na sio kushambuliana baina ya vyama wala
vyama na serikali.
Jaji Mutungi ameyasema hayo Leo wakati akitoa salamu maalum za mwaka mpya kwa vyama vya siasa na watanzania wote.
"Unajua siasa na wana siasa lazima wakomae sasa, siasa za
kizamani zilikuwa hazinogi kama hakuna kurushiana vijembe, kejeri na
Matusi. Sasa hivi mambo hayo yameshapitwa na wakati na wanasiasa hasa
wanaowanadi wagombea wao wahakikishe wanatumia Muda mwingi Zaidi kunadi
sera zao kuliko kushambuliana". Alisema Mutungi
''...unajua siasa.......siasa za chuki zinazogubikwa nakurushiana vijembe....zimeptwa na wakati....''liongeza Jaji Mutungi
JAMVI LA HABARI lilipotaka kujua ni nini ofisi yake
inawaahidi watanzania na wafuatiliaji wa siasa kwa mwaka huu mpya 2017
tuliouanza juzi, Jaji Mutungi ameahidi kuendelea kutoa huduma Sawa kwa
vyama vyote vya siasa hapa nchini kwa kuwa ofisi yake ina wajibu wa
kuvilea vyama hivyo na Demokrasia. ...
kadharika jaji mutungi ameahidi kuendelea
kudumisha ukuaji wa demokrasia nje na ndani ya vyama na kuvikumbusha
vyama kujiendesha kama taasisi na kuhimiza vyama kufuata katiba zao na
si matakwa ya Viongozi pasipo kuzingatia matakwa ya katiba zao.
nakala ya Calender ya mtandaoni iliyotolewa na msajili wa vyama vya siasa
0 comments: