NI ZUMA NA BUHARI, MARAIS WA KWANZA WA AFRIKA WALIOZUNGUMZA NA TRUMPAT
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari leo
hii akiwa mjini London amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Marekani
Donald Trump, kufuatia ombi kutoka kwa rais huyo wa Marekani.
Viongozi hao wawili walizungumzia njia za kuboresha ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi.
Trump alimshauri Rais Buhari kuendelea na kazi nzuri anayoifanya na pia kumpongeza kwa jitihada alizofanya za kuokoa wasichana 24 wa Chibok na hatua zinazopigwa na jeshi la Nigeria.
Trump alimhakikishia rais huyo wa Nigeria kuwa Marekani iko tayari kuafikiana na Nigeria kuhusu suala la kuisaidia na silaha ili iweze kukabiliana na ugaidi.Rais Trump pia amemualika Buhari kwa ziara nchini Marekani.
Baadaye Trump pia alifanya mazungumzo ya simu na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. Viongozi hao walikubaliana kufanya jitihada za kuboresha zaidi ushirikiano mzuri uliopo kati ya mataifa hayo mawili.
Zuma alimpongeza Trump kwa kuchaguliwa kuwa rais wa 45 wa Marekani.
Kunazo kampuni 600 za kimarekanai nchini Afrika Kusini na pia ushirikiano mzuri wa kibiashara kati ya mataifa hayo.
Marais hao pia walijadili umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja katika masuala kadha ya kuhakikisha kuwepo amani barani la Afrika.
0 comments: